Ukosefu wa mazoezi kwa watoto huathiri afya zao hivyo kuwafanya wawe dhaifu ukubwani

Ukosefu wa mazoezi kwa watoto huathiri afya zao hivyo kuwafanya wawe dhaifu ukubwani

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,060
Habari!

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, watoto wanne kati ya watano wenye umri wa miaka 11-17 duniani hawafanyi mazoezi ya viungo ya kutosha.

Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuwa afya za watoto zinaharibiwa kutokana na ukosefu wa mazoezi hivyo kuathiri ukuaji wa ubongo na shughuli zao za ujuzi kupungua uwezo.

Utafiti huo umesema kwamba chanzo ni kutokufanya mazoezi, inashauriwa kuwa ni vyema mtoto kufanya mazoezi walau kwa saa moja kwa siku.

Tatizo hili limekuwa kubwa duniani kote katika mataifa maskini na tajiri.

Watoto wa kiume wanaonekana kujishughulisha zaidi katika kufanya mazoezi kuliko watoto wa kike katika nchi 4 kati ya 146 zilizofanyiwa utafiti.

Inashauriwa watoto kufanya mazoezi yoyote yanayofanya mapigo ya moyo yaende kwa haraka na mapafu kupumua kwa nguvu, kama vile;

  • Kukimbia
  • Kuendesha baiskeli
  • Kuogelea
  • Kucheza mpira
  • Kuruka kwa mguu mmoja
  • Kuruka kamba
  • Sarakasi n.k.

1574527983395.png


Kwa undani zaidi wa makala hii pitia:
 
Back
Top Bottom