2013
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 11,360
- 6,069
Vipindi vingi vya Dini hususani vya Kikristo katika radio mbalimbali nchini vinaendeshwa na watangazaji ama wasemaji wasioweza kuzungumza lugha fasaha ya kiswahili. Inaonyesha hata wanao wasaili hawajui kama hawajui kiswahili Sanifu.
Mfano, Unakuta mtangazani anatakiwa aseme Roho Mtakatifu anasema loho Mtakatifu, lehema, balikiwa, kilisto(kristo)kilisimasi(,krismasi), balaka(Baraka). Zabuli/(Zaburi),msaraba(msalaba) kuwekwa Ulu(Huru).
Etc.
Ukiondoa Roman Catholic, vyombo vilivyobaki ni kama Ushabiki tu linapofika swala la kutangaza Kwa kiswahili sanifu. Jambo linaloongeza kero na kutoamini inapotokea unatakiwa kumsikiliza mtu asiyejua Nini anazungumza. Ni jambo lililo Dhahiri kwamba Wako watu wasioweza kuvumilia kumsikiliza mtu anayezungumza vibaya. Athari zake ni kusababisha radio kutopendeza wengi na kukosa wafuatiliaji.