Ukosekanaji wa Mafuta Je EWURA mnasema ukweli

Ukosekanaji wa Mafuta Je EWURA mnasema ukweli

Maendeleo tu

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2010
Posts
347
Reaction score
107
Ndugu zangu Watanzania, kwanza poleni kwa changamoto zinazojitokeza kwa ukosekanaji wa mafuta. Tunaona juhudi mbalimbali zinafanywa kuondoa tatizo la mafuta. Jana na leo asubuhi tuliweza kumuona bwana Maswi akitoa miongozo na makemeo kwa wauzaji na chombo kinachodhibiti "EWURA" kuhakikisha wote walioyabana mafuta wanayatoa na kuyauza pamoja na kuhakikisha yanakuwepo nchi nzima.

Hebu tujiulize kidogo, hivi kama baadhi ya watendaji wa EWURA haohao pia wanamiliki vituo vya kuuzia mafuta na wanajua bei zitapanda lini, wanaweza kujiadhibu kweli au hata kujikemea??? Huu ndiyo msingi wa swali langu kama EWURA ni wakweli juu ya ukosefu wa mafuta au ndiyo changa la macho kama kawa...

Wadau mnasemaje??
 
Wakubwa wa EWURA wamo kwenye payroll ya matajiri wa mafuta, msitarajie lolote kutoka kwa jibwa koko, lili kibogoyo
 
We utaona... Wanagoma kwa sababu siku za kuweka bei elekezi ziko karibu sasa wanatengeneza uhaba makusudi ili bei ikija itakuwa imepanda na wao kuchuma faida kubwa . ANGALIZO.... EWURA hawana sababu yoyote ya kupandisha bei maana hata kwenye soko bei imeshuka kdg na pia shilingi yetu imekaa palepale bila kushuka kwa muda mrefu.
 
The more corrupt the state, the more numerous the laws...
 
Tatizo la uhaba wa nishati ya mafuta lina zaidi ya week, viongozi wako ofisini wanaona na hawachukui hatua, kaaaa!!!!!!!! Inasikitisha sana, wanakula good time wananchi tunapata shida, wao hhhaaa!!!! Roho kwatu!!! No one cares for what is happening to the natives of this country especially when leaders’ positions are not endangered!!!,


Watu wanataabika kupata bidhaa ambazo zipo ghalani, uongozi wa nchi upo unaangalia tuuuu!!!!!!!! Tatizo la mafuta hapa Bongo kwani limeanza jana au leo!! Uhuni huu wa wauza mafuta una zaidi ya wiki sasa, watu wanapata shida, wanakaa kwenye foleni toka saa 11 alfajiri (huku Singida mpaka saa 5 asb halafu unaambulia lita 5 tu) ili kupata hiyo nishati lakini wapi hali ni ngumu kuliko maelezo, hii siyo sawa kabisa!!!, sisi wengine tumesafiri zaidi ya kilimeta 70 mpaka Singida mjini kufuata mafuta, tukaambulia sifuri, Viongozi wapo wakula good time wako maofisini wanapata viyoyozi ambavyo hata bili yake ya umeme na mafuta yaliyompeleka pale ofini yanatokana na kodi zetu ila wao wametuli tuli as if nothing is happening in the country.


Hivi hili limnyama linaloitwa intelegencia (kumbuka lilitajwa kwa msisitizo na IGP Mwema) huwa linafanya kazi kutetea maslahi ya kisiasa tu, tena kwenye maandamano ya CUF and CDM tu? Hivi halifanyi kazi kuchunguza kinachoendelea katika nchi ikiwa ni pamoja ni mipango ovu kama hhii inayoathiri uchumu wan chi? Wanaojua tupia majibu hapahapa JF.


Viongozi wa Tanzania mnataka nini kitokee ndipo mchukue hatua za haraka? Watu waandamane ndipo mjue kuna shida? Kwanini mnakuwa wagumu kuchukua hatua haraka? Kwanini mnakuwa wagumu kusimamia maamuzi yenu? Mnabaki kuuza wananchi tena maskini na walalahoi. Mnakaa zaidi ya week kuchukua maamuzi, Hivi ni nani huwa anawakataza kuchukua mamuzi sahihi kwa wakati muafaka? Ni nani? Mtajeni, Rais wangu JK mtaje anayekuzuia wewe kuchukua maamuzi? Kwanini lkn? Why?


Jamani niwakumbushe wale mliosahau, wakati serikali ya Rais JK imeingia madarakani 2005, waliliona tatizo hili la uhaba wa mafuta, pia waliona na kujua uhuni unaofanywa na wauza mafuta nchini Tanzania. Wakaamua na kututangazia wananchi kuwa sasa serikali itakuwa na utaratibu wa kununua mafuta kutoka ughaibuni na itakuwa visima vyake kuzia wananchi hiyo bidhaa kwa kutumia NDC, baadaye tukataarifiwa kuwa fedha tayari zimetengangwa kwa kazi hiyo. Sasa cha kushangaza mpaka sasa nothing has been done, leo uhuni bado unaendelea na hakuna hatua zinazochukuliwa na serikali ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu.

Ni nani alimkataza Rais Jakaya Kikwete kuendelea na mpango wake wa kununua mafuta kwa ajili ya raia wake? Nauliza tena nani alimkataza Mh.Kikwete kununua mafuta?

Kama hakuna, Rais Jakaya Kikwete anamwogopa nani katika nchi hii ktk kutekeleza maamuzi ya serikali yake?

kwanini mafuta hayanunuliwi na serikali?

Na Je, zile pesa zilizotengwa kwa kazi hiyo sasa zilifanya kazi gani?


Swali lingine la nyongeza, kwanini wafanyabiashara wa mafuta wanaogopwa sana na serikali hii?, kumbuka Mh. Rais Jakaya Kikwete unakumbuka uliongeza bei ya mafta ya taa kwa kuwaogopa wachakachuaji wa mafuta, hapa mliona kheri Mwananchi mlalahoi aendelee kuuzwana kupuuzwa na kubamizwa bei ya mafuta ya taa kuliko kumkamata mchakachuaji.

maswali yangu haya sasa yananikosesha majibu yake, mwenye majibu anipe hapahapa JF, mie ni mlalahoi lakini mwenye ufahamu.
Naomba tuwe wazalendo wa kweli kwenye taifa hili, vinginevyo tunakaribisha fujo katika nchi na hili lazima lianzie kwenu viongozi wa juu, mwangwi wenu tuusikie huku chini
 
Back
Top Bottom