Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Gavana, Viacheslav Chaus, alitumia programu ya kutuma ujumbe ya Telegram kukashifu ahadi ya Urusi.
"Urusi yaanzisha mashambulizi mapya baada ya ahadi ya amani, Tunaamini ndani yake? Bila shaka sivyo," alisema, akiongeza Urusi ilikuwa imeshambulia Chernihiv "usiku kucha".
Siku ya Jumanne, Urusi ilisema itapunguza shughuli karibu na Chernihiv na mji mkuu, Kyiv. Ving'ora vya mashambulizi ya anga vilisikika mjini Kyiv mapema Jumatano, saa chache baada ya Urusi kusema kuwa itaondoa baadhi ya wanajeshi katika mji mkuu.
Naibu meya wa Kyiv, Mykola Povoroznyk, alikanusha Mji Mkuu kushambuliwa na makombora, ingawa milio ya risasi ilisikika kutokana mapigano na mapigano yanayoendelea karibu na jiji hilo.
Maafisa wa Marekani na Ukraine wanasema Urusi inaendelea kuweka vikosi vyake mbali na Kyiv, pengine kama sehemu ya juhudi za kuangazia tena maeneo ya mashariki.
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Russia, Alexander Fomin, alisema nchi hiyo "itapunguza kwa kiasi kikubwa, mara kadhaa shughuli za kijeshi" katika juhudi za "kuongeza uaminifu" katika mazungumzo ya amani.
Wajumbe kutoka Moscow na Kyiv walifanya mazungumzo ya saa tatu mjini Istanbul siku ya Jumanne yaliyolenga kuhitimisha mapigano ya zaidi ya mwezi mmoja nchini Ukraine.
Ukraine ilisema kuwa imependekeza kuwa taifa lisiloegemea upande wowote katika ujihakikishia usalama. Lengo kuu la uvamizi wa Urusi lilikuwa ni kusimamisha Ukraine kujiunga na muungano wa Nato na maafisa wa Urusi walisema kuwa mazungumzo hayo yamefikia hatua ya kivitendo.
Chanzo: BBC