Raphael Thedomiri
JF-Expert Member
- Sep 1, 2019
- 442
- 729
Urusi imesema idadi ya vifo vya wanajeshi wake kufuatia shambulizi la Ukraine kwenye mkesha wa Mwaka Mpya katika eneo la Makiivka imepanda hadi 89.
Moscow imesema mapema leo kuwa miili zaidi ilipatikana kwenye vifusi katika mji wa Makiivka ulioko mkoa wa mashariki wa Donetsk unaodhibitiwa na Urusi.
Wizara ya Ulinzi imesema mkasa huo ulitokea kwa sababu askari wa Urusi walitumia simu za mkononi, na hivyo kufichua mahala walikokuwa kwa wanajeshi wa Ukraine.
Urusi ilisema Jumatatu kuwa wanajeshi wake 63 waliuawa, ikiwa ndio idadi kubwa kabisa ya vifo kutokana na shambulizi moja tangu kuanza kwa vita vyake Februari mwaka jana.
Ukraine iliishambulia kambi ya muda ya Urusi katika mji wa Makiivka Januari mosi usiku wa manane kwa kutumia mifumo ya makombora ya HIMARS yanayotolewa na Marekani.
Ukraine inasema idadi ya vifo huenda ni kubwa zaidi kuliko inavyoripotiwa.
Dw