Nilishawahi kusema kuwa mwisho wa siku Zelensky na Ukraine yake watajakuwa maadui wakubwa sana wa Marekani na NATO kwa ujumla.
Kisa ni kwamba haiwezekani kuipatia Ukraine kila inachokitaka bila kuangalia athari yake kwa usalama wa dunia! Kwa mfano Zelensky alikuwa anataka NATO waweke NO FLY ZONE nchini ukraine. Kwa maana ya kwamba NATO wawe tayari kulilinda anga la ukraine dhidi ya ndege za kivita za urusi!!
Urusi ikasema huo ni mstari mwekundu!! Ukiamua kuuvuka ujiandae vizuri maana LAZIMA kipigo lipizi kifuatie!! Na Marekani haiko tayari kuhatarisha maisha ya watu wake hata mmoja!! Mara 100m ukraine wote waangamie kuliko mmarekani mmoja auawe! kwa hiyi NATO walisema HAPANA kwa ombi la no fly zone!!
Ombi lingine la ukraine kwa Marekani ni kupatiwa vifaa vizito vinavyoweza kurusha makombora ya masafa marefu hadi ndani kabisa ya urusi!! Na Marekani walikuwa wamekubali kupeleka makombora hayo, lakini Urusi ikasema HUO NAO NI MSTARI MWEKUNDU!!
Ukipeleka makombora ya masafa marefu ukraine utakuwa umeuvuka mstari mwekundu wa urusi kinachofuatia hapo siyo majadiliano ila KIPIGO!! Kuona hivyo ghafla Marekani ikabadili gia angani na kusema haitapeleka makombora ya masafa marefu ukraine.
Hasira za Ukraine zikaanzia hapo, Zelensky akamtuma msaidizi wake apeleke salamu kwa marekani kwamba "isipopewa makombora hayo ya masafa marefu ITAIBWATUKIA Marekani kwa BWATUKO la mfano!!
Bwatuko hilo ni mithili ya mtu aliyechanganyikiwa au mtoto aliyedekezwa siku wazazi wakamnyima kitu anachokitaka, waingereza huliita bwatuko hilo kama "exemplary tantrum"
Maana ya tantrum kwa mujibu wa kamusi: Tantrum definition, a violent demonstration of rage or frustration; a sudden burst of ill temper.
Zelensky aide pressures US
Presidential aide Alexey Arestovich has threatened Washington with an ‘exemplary tantrum’ over non-supply of rocket artillery systems
Zelensky aide pressures US.
Kiev will resort to hysterical outbursts, if the US fails to deliver multiple rocket launchers to fight Russia, an aide to President Volodymyr Zelensky said on Monday. Alexey Arestovich was responding to remarks by US President Joe Biden, who said the US won’t send to Ukraine long-range rockets that can hit Russia.
Washington is reportedly on the brink of stepping up the arming of Ukraine with heavier weapons. Arestovich, a key figure in Ukraine’s messaging on military affairs, outlined Kiev’s response to a scenario, in which the weapons are not delivered as expected.
Swali la kujiuliza ni je Marekani itaitikiaje BWATUKIO la Ukraine ukizingatia kuwa Marekani imeibeba sana Ukraine kifedha na kisilaha na mafunzo toka 2014 hadi sasa. Halafu shukrani yake iwe ni bwatukio la mfano!! Kusema ukweli bila Marekani kuibeba ukraine kwa fedha, silaha na kidiplomasia hivi vita vingeshaisha siku nyingi!! Mwisho wa siku Marekani na Ukraine watahasimiana sana!!
Marekani itaiona Ukraine kuwa haina shukrani na haina adabu. Kwanza kitendo cha kutishia kuibwatukia Marekani ni kwamba tayari imeshaibwatukia! Lakini kwa upande mwingine, Ukraine itaiona Marekani kuwa imewaingiza mkenge kuwasukumizia kwenye mdomo wa Urusi almaarufu kama DUBU MWEKUNDU/RD BEAR!! Ukraine ilirubuniwa na Marekani kuivimbia Urusi na ikatae kutekeleza makubaliano ya amani ya Minsky!
Ukraine ilipewa kiburi kuwa itaingizwa fasta NATO kwa hiyo Urusi haitothubutu kuigusa!! Kwa hiyi ukraine ilipotakiwa na Urusi kuachana na mipango ya kujiunga NATO iligoma!! Ikijua kwamba Urusi ikijaribu kushambulia NATO itaingilia kati.
Pia Ukraine iliahidiwa kujiunga EU fasta. Mambo yote mawili hayakutimia!! Haikujiunga NATO wala EU na huo uwezekano HAUPO katika siku za karibuni!! Yawezekana kuna uongo mwingine aliodanganywa ukraine na haujajulikana bado kwa hiyo Ukraine anatishia atauweka wazi, hiyo inaitwa BLACKMAIL!! Kama ni hivyo Marekani ana wakati mgumu sana!! Ngoja tuone itakavyokuwa!!
Kwenye uwanja wa mapambano ndo hivyo tena hata sarakasi za comedy kwa Zelensky zimeishia, ni kilio muda wote!! Kipigo cha mrusi huko DONBAS siyo cha kitoto!!