Ukraine yajiandaa kwa vita vya kemikali, Marekani yatoa usaidizi

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257

Imeripotiwa kuwa Marekani imekuwa ikituma vifaa vya kinga (PPE) kwa Ukraine kwa ombi la nchi hiyo ili kujiandaa kwa shambulio lolote la silaha za kemikali wakati wa vita dhidi ya Urusi inayoendelea.

Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Rais Joe Biden alithibitisha kwamba "vifaa vya kuokoa maisha" vimetumwa.

PPE inadhaniwa kujumuisha barakoa za gesi, suti za hazmat na vifaa vingine.

Ni kiasi gani ambacho Marekani inapanga kutuma haikufahamika mara moja, lakini msemaji huyo alisema "msaada huu hauhatarishi utayari wetu wa ndani".

Moscow na Magharibi zimerushiana tuhuma katika wiki za hivi karibuni kwamba silaha za kemikali na silaha za kibaiolojia zinaweza kutumwa.

Maafisa wa Marekani wanahofia kuwa Urusi inaweza kuwa inapanga operesheni ya uwongo ya bendera kuhusu matumizi ya silaha hizo.


Chanzo: BBC
 
Hii ni vita mbaya kuliko vita ya nuclear. And its not heathy war

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Safi kabisa kazi iendelee., wale waliosema Ukraine wanaomba poo kumbe ndio kwanza wazee wa Stinger wanapiga Ant-chemical, putini akajiandae na sasa hizo zitagawiwa mpaka kwa watoto wa shule
 
Vita haina Silaha Maalum,Sasa kama wewe una Rungu mimi nna Bunduki nifanye nini?Nakumwaga Uharo tu.
Mimi natamani Ukraine atumie hizo chemical zao ili warusi watumie nuclear zao vzr maana zimekaa stop tu zikipigwa vumbia miaka nenda miaka Rudi.

Yajayo yanafurahisha.
 
Habar mbaya ni kwamba phase one ni kushambulia ukrain after all kibao kinageuka zamu ya urus kushambuliwa wameanza na ghala lamafuta ni show show
 
Vita haina Silaha Maalum,Sasa kama wewe una Rungu mimi nna Bunduki nifanye nini?Nakumwaga Uharo tu.
... Russia inayosifika duniani kote katika medani za kivita na kijasusi ndio ya kumwaga uharo kweli? Kumbuka medani za kijasusi zimethibitisha anayeenda kuharisha ni Putin.
 
Wimbo lingine la Covid... Propaganda...
 
Mimi natamani Ukraine atumie hizo chemical zao ili warusi watumie nuclear zao vzr maana zimekaa stop tu zikipigwa vumbia miaka nenda miaka Rudi.

Yajayo yanafurahisha.
Miaka ya mababu zetu watu walipigana vita lakini wakiacha mazingira salama, mapanga, visu, mikuki na ngumi havichafui mazingira.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…