Tukiona DRC kajisalimisha kwa USA ili asaidiwe kuwaondoa M23 tusishangae! Je, Putin atakuwa ameingiwa ubaridi sasa?
Habari kamili;Ukraine imekubali masharti ya mkataba mkuu wa madini na Marekani, afisa mkuu wa Kyiv ameiambia BBC. "Kwakweli tumekubaliana na marekebisho kadhaa mazuri na tunaona kama matokeo ni chanya," afisa huyo alisema, bila kutoa maelezo zaidi.
Ripoti za vyombo vya habari zinasema Washington imepunguza madai ya awali ya haki ya $500bn (£395bn) katika mapato yanayoweza kutokana na kutumia maliasili lakini haijatoa hakikisho dhabiti la usalama kwa Ukraine iliyokumbwa na vita ambalo ni hitaji kuu la Ukraine.Bila kuthibitisha kuwa makubaliano yamefikiwa, Trump alisema Jumanne kwamba kwa malipo ya makubaliano hayo Ukraine itapata "haki ya kupigania".
Rais wa Marekani Donald Trump alisema anamtarajia mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Washington kutia saini mkataba huo wiki hii, baada ya viongozi hao wawili kurushiana maneno makali.
"Wao ni wajasiri sana," aliwaambia waandishi wa habari, lakini "bila Marekani na pesa zake na zana zake za kijeshi, vita hivi vingekuwa vimeisha kwa muda mfupi sana".
Alipoulizwa kama usambazaji wa vifaa vya Marekani na risasi kwa Ukraine utaendelea, alisema: "Labda hadi tutakapokuwa na mpango na Urusi... Tunahitaji kuwa na makubaliano, vinginevyo yataendelea."
Chanzo; BBC Swahili