Ukraine yalalamika Russia kutumia makombora hatari ya thermobaric rockets, wachambuzi wa silaha wa USA wasema huo ni 'ukatili'

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2019
Posts
2,926
Reaction score
15,634
Ukraine inalalamika kuwa Russia inatumia silaha nzito mno, TOS-1A Thermostatic Rockets (vacuum bombs), ktk mapigano huko Donetsk.

Kwa mujibu wa Marekani, silaha hizo ni special kwa kuangamiza ngome za kijeshi zilizo kwenye mahandaki chini ya ardhi na maadui waliojificha kwenye bunkers. Silaha hizo zinapotumika huwa hakuna kitu kinachoweza kumkinga mtu na mlipuko wa silaha hizo.

Wachambuzi wa maswala ya silaha wa Marekani wanasema Russia kutumia silaha hizo dhidi ya majeshi ya Ukraine ni ukatili tu.

Wachambuzi hao wa Marekani wameendelea kukazia kuwa pamoja na kuwa kwa sasa hakuna sheria zinazozuia matumizi ya silaha hizo za Russia (TOS-1A thermobaric rockets), lakini maangamizi yanayosababishwa na silaha hizo hupelekea baadhi ya wachambuzi wa maswala ya silaha kuweka matumizi ya silaha hizo katika makosa ya uhalifu vitani.

Omusolopogasi na Glenn (waMarekani wetu wa Nanjilinji) njooni hapa mteseke tena zaidi

=====



 
Zelensky kawaingiza waUkraine cha kike. Akubali kushindwa na aondoke madarakani maisha ya wananchi wa Ukraine yaendelee. Kukubali kupambana na russia kupitia vimisaada vya silaha toka Western ni kutaka kuifanya ukraine iharibike zaidi.
 
Juzi walisema Russia anatumia silaha dhaifu, jana wakasema Russia anatumia silaha za zamani yaani vifaru vya miaka hamsini iliyopita.

Leo tena wanasema anatumia silaha kali mno...sasa tuwaeleweje hawa watu.
Katumia dhaifu wanapiga kelele, kaamua atumie za zamani anaona bado Majeuri sasa anatumia vya kisasa[emoji1783][emoji1783][emoji1783]
 
Zelensky kawaingiza waUkraine cha kike. Akubali kushindwa na aondoke madarakani maisha ya wananchi wa Ukraine yaendelee. Kukubali kupambana na russia kupitia vimisaada vya silaha toka Western ni kutaka kuifanya ukraine iharibike zaidi.
Kwa nini unakuwa mnafiki? Russia wamefuata nini kwenye nchi ya watu.
 
Weka link ya habar yako tukasome wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…