Narumu kwetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 1,888
- 4,489
Chanzo cha picha: Getty Images
Maelezo ya picha,Kyiv hapo awali iliweza tu kutumia makombora hayo ndani ya mipaka yake. Ukraine imerusha makombora ya Storm Shadow yanayotolewa na Uingereza kulenga shabaha ndani ya Urusi kwa mara ya kwanza, BBC imeelezwa.
Nchi hiyo inayokumbwa na vita hapo awali iliwekewa vikwazo vya kutotumia makombora ya masafa marefu nje ya mipaka yake.
Taarifa za mashambulio hayo zimekuja baada ya Ukraine kupewa kibali kutoka Washington cha kurusha makombora yaliyotolewa na Marekani ndani ya ardhi ya Urusi. Serikali ya Uingereza imekataa kutoa maoni kuhusu ripoti hizo, lakini maafisa wamethibitisha kwamba Waziri wa Ulinzi, John Healey alizungumza na mwenzake wa Ukraine Jumanne usiku.
Mawaziri huenda wakachukua tahadhari katika majibu yao kwa ripoti hizo kutokana na wasi wasi juu ya majibu ya Urusi, pamoja na kuhakikisha hatua hiyo haionekani kuwa inaongozwa na Uingereza.
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Rustem Umerov pia amekataa kuthibitisha kwamba nchi yake imetumia makombora ya Storm Shadow kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi, lakini amesema "tunatumia njia zote kuilinda nchi yetu."
Matthew Miller, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alipoulizwa na BBC ikiwa Ukraine inashauriana au kuifahamisha Marekani kuhusu matumizi ya makombora yaliyotolewa na Uingereza, Bw Miller amesema hatazungumza hadharani kuhusu matumizi ya silaha za nchi nyingine.
Rais Volodymyr Zelensky ametoa wito mara kwa mara kwa washirika wake wa Magharibi kuidhinisha matumizi ya makombora ya masafa marefu dhidi ya shabaha ndani ya Urusi, akisema ndiyo njia pekee ya kukomesha vita.
Kombora la Storm Shadow linachukuliwa kuwa silaha bora ya kupenya mahandaki magumu na ghala za silaha, kama makombora yanayotumiwa na Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukrain