KWELI Ukraine yashambulia mji ambao rais Samia atahudhuria mkutano wa uchumi na Putin huko st petersburg nchini urusi

KWELI Ukraine yashambulia mji ambao rais Samia atahudhuria mkutano wa uchumi na Putin huko st petersburg nchini urusi

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Kumekuwepo na chapisho ambalo limechapishwa kwenye mtandao wa instagram likiwa na nukuu ambayo inasema kuwa ukraine yashambulia mji ambao rais samia atahudhuria mkutano na putin huko st petersburg nchini urusi
je uhalisia wa video hiyo ni upi ?
IMAGE.jpg
 
Tunachokijua
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya ziara kuelekea nchini Urusi Juni 2, 2026 ambapo kupitia ukurasa wake wa X aliandika:

"Nimeondoka nchini leo kuelekea Shirikisho la Urusi kwa ziara ya Kitaifa kufuatia mwaliko wa Mheshimiwa Rais Vladimir Putin, ikiwa ni ziara ya pili kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya ile ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Oktoba 1969"

Madai

Kupitia baadhi ya mitadao ya kijamii ikiwemo Instagram kumekuwapo na video iliyoambatanishwa na ujumbe unaosomeka "Ukraine shambulia mji ambao Rais Samia atahudhuria na Putin huko St. Petersburg nchini Urusi".

Uhalia wa madai hayo.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejirirdhisha kuwa ni kweli Ukraine ilishambulia kwa ndege zisizo na rubani katika visima vya mafuta katika mji wa St. Petersburg huko nchini Urusi. Vyanzo mbalimbali vilichapisha taarifa hiyo Juni 3, 2026. Tovuti ya ABC iliandika,

"Droni hizo zilisafiri umbali wa zaidi ya kilomita 1,000 (maili 600) ili kupiga kituo hicho, alisema Zelenskyy kwenye mitandao ya kijamii. Mawingu ya moshi mweusi yalipanda juu ya bandari ya mji huo baada ya shambulio hilo. St. Petersburg ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Urusi na ndipo alipozaliwa Putin."
Back
Top Bottom