The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Ukraine imerejesha nyumbani miili mingine 1,200 iliyokabidhiwa na Urusi, hatua mpya katika makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo ya hivi majuzi kati ya pande zinazozozana mjini Istanbul, taaasisi ya serikali ya Ukraine inayohusika na suala hilo
Ukraine imepokea miili mingine 1,200 ambayo, kulingana na upande wa Urusi, ni ya raia wa Ukraine, pamoja na wanajeshi," Kituo cha Uratibu cha Wafungwa wa Vita cha Ukraine kimetangaza kwenye Telegram.
Wakati wa mazungumzo huko Istanbul, Uturuki, mwanzoni mwa mwezi Juni, Kyiv na Moscow zilikubali kuwaachilia wafungwa wao wote wenye umri mdogo au waliojeruhiwa na kurudisha miili ya wapiganaji waliouawa, matokeo pekee yanayoonekana ya mazungumzo haya.
Tangu wakati huo, pande hizo mbili zimefanya duru tatu za kubadilishana wafungwa, huku Ukraine ikipata miili 1,212 siku ya Jumatano na mingine 1,200 siku ya Ijumaa, na kuifanya kuwa moja ya operesheni kubwa zaidi tangu mashambulizi ya Urusi yaanze mnamo 2022.
Kwa upande wake, Urusi ilmeripoti kupata miili 27 ya wanajeshi wa Urusi waliouawa waliokabidhiwa na Ukraine siku ya Jumatano. Haikutoa tangazo lolote kuhusu shughuli za Ijumaa na Jumamosi.
Kurejeshwa kwa miili ya kijeshi na kubadilishana wafungwa wa vita ni nyanja chache ambazo Kyiv na Moscow zimeshirikiana tangu kuzuka kwa vita, lakini mwishoni mwa wiki iliyopita, nchi hizo mbili zilishutumu kila mmoja kwa kuzorotesha zoezi hilo.