Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Nimemuongelea Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.Tuanzie hapa,
Nadhani anatafutwa hapa Mungu muumba wa kila kitu. (Hata mema na mabaya)
Yaani Mungu muweza wa yote, asiyeshindwa lolote.
Km anaweza yale wewe unayoona kuwa ni mema hawezi kushindwa hata yale unayoona kuwa ni mabaya.
Maana asipoweza lolote kati ya hayo anakuwa kapungukiwa sifa yake ya uungu.
Labda km tukajadili imani, huo ni mjadala mwingine.
Hapo bado hujathibitisha kuwa hayupo"
Pia Mungu huyo ana haki yote.
Mungu huyo ni wa kufikirika tu.
Huyo Mungu anafikirika na kusemeka, lakini hayupo.
Ni kama wewe unavyoweza kuifikiria na kuisema "pembetatu ambayo pia hapo hapo ni duara". Unaweza kuifikiria, unaweza kuisema. Lakini, ukiweza kuifikiria na kuisema, hilo halimaanishi ipo.
Kwa nini pembetatu ambayo pia ni duara haipo? Kwa sababu dhana ya kuwapo hiyo pembetatu ina internal contradiction. Inajipinga yenyewe. Pembetatu haiwezi kuwa duara, na duara haliwezi juwa pembetatu.
Hivyo hivyo, Mungu mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya ni contradiction.
Kwa sababu upendo wake wote hauendani na yeye kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya. Hii ni pembetatu duara, ni contradiction.
In fact, sihitaji hata kwenda kwenye Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote kuona contradiction.
Nikichukua tabia ya "muweza yote" tu, ambayo umeotaja wewe, tayari ina contradiction.
Je, Mungu muweza yote anaweza kuumba jiwe ambalo litakuwa zito sana kiasi ashindwe kulibeba?
Ukisema ndiyo, anaweza, tayari ushakubali huyo Mungu hawezi yote, kwa sababu kuna jiwe anaweza kuliumba akashindwa kulibeba.
Ukisema hawezi kuliumba hilo jiwe, kwa sababu anaweza kubeba kila jiwe, ushakubali kwamba hawezi yote, kwa sababu kuna hilo jiwe hawezi kuliumba.
Kwa hiyo tunaona hata hii sifa ya "muweza yote" ni sifa ya kufikirika tu, kimantiki inazaaa contradictions.
Kwa hivyo, tumeona kuwa.
1. Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya ni contradiction. Ulimwengu kuweza kuwa na mabaya kunaonesha Mungu huyo hayupo.
Umesema Mungu anaweza yote mema na mabaya, lakini nikakuonesha Mungu mwenye upendo wote kuruhusu mabaya ni contradiction. Mabaya kuwepo ni ushahidi na uthibitisho kwamba Mungu huyo hayupo.
2. Tumeona kuwa hata tukiondoa sifa za mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, sifa ya muweza yote yenyewe ni ya kufikirika, haiwezekani kuwapo kimantiki. Tumeona Mungu muweza yote akipewa mtihani wa kuumba jiwe zito kiasi asiweze kulibeba, sifa yake ya kuweza yote lazima itavunjika. Akiweza kuliumba hilo jiwe, sifa ya kuweza yote itavunjika kwa sababu atashindwa kulibeba. Asipoweza kuliumba hilo jiwe, sofa ya kuweza yote itavunjika kwa sababu hataweza kuliumba hilo jiwe. Kwa hivyo kuweza yote ni sifa ya kufikirika tu, kimantiki haiwezi kuwepo na Mungu muweza yote hawezi kuwapo.
Umeelewa? Au bado una ubishi?