Ukristu wazidi kuenea kwa kasi Indonesia

Acha kuhangaika, Quran ni ileile hizo ni porojo zenu za kutaka kuifananisha Quran na Bible,ibn batuta alifika kilwa 1300,akaikuta Quran hiihii,nimekupa notes za birmingham university,Quran hiihii, familia ya kifalme uingereza ilirudisha nakala ya Quran iliyokua nayo muda mrefu,nakala hiyo ilipokaguliwa haina tofauti na hizi zilizopo
 
We ziite porojo tu ila tafuta data na uujue ukweli, Yassir kadhi mmoja wa the best Quranic scholars toka Harvard university anasema hiyo standard narrative has holes in it .

Walimu wenu wa madrasa wanawalisha matango pori kwa kuleta story za kwamba Quran haujawahi badilika neno kwa neno.
 
Mkuu narudia tena hii saveMaryam nimeitembelea juu chini ni blog na page na ya mtu binafsi ipo facebook lengo lake ni kuuchafua uislam, kama una website ama link nyengine lete hapa tuone waislam milioni 2 Indonesia waingia ukiristoni kila mwaka.
Sasa hayo ni mawazo yako binafsi na sio ya kitafiti huko kusema lengo lake ni kuuchafua uislamu ni kama Kuna kivuli unakitengeza ili ujifiche

Mimi angalau nimekuletea hata page yao inayosapiti Islam awakening movement, basi wewe Lete ushahidi unaoonesha hii taasisi si ya kiislamu au Lete ushahidi wowote unaoonesha waislamu wa Indonesia wameipinga SaveMaryam

Usikimbilie kutengeneza vichaka vyako leta ushahidi unaodhihirisha hoja zako
 
Yaani habari za Quran unaleta story za mhadhiri wa havard!!..acha ujinga
 
Acha uongo na uzushi! Qur'an ni ileile!

Unachojaribu kukipotosha tayari historia yake imo haijafichwa wala si kitu cha kustaajabisha. Kwenye sahihi bukhari historia yake ipo!

Na kwa taarifa yako aliyeikusanya Qur'an yaani physical collection si Khalifa Uthman, aliyeikusanya Qur'an ni Khalifa Aboubakr Siddiq.

Hii ilitokana na hifdhi wa Qur'an wengi kuuliwa kwenye vita vya Alyamamah.

Sahaba Umar Ibn Al Khattwab alimshauri sahaba mwenzie Aboubakr Siddiq Qur'an yote ikusanywe na iwekwe kwenye mfumo wa maandishi.

Aboubakr Siddiq ambaye ni Khalifa wa kwanza wa Mtume swallallahu alayhi wasalllam aliwakusanya pamoja masahaba wote waliyokuwa wameisoma Qur'an na kuikariri kwenye vifua vyao na vipande vilivyokuwa vishaandikwa, na aliandaa kamati na kuikusanya Qur'an pamoja na kuiandika.

Hivyo kitabu kiitwacho mas-haf kilitokea. Elfu thelathini na tatu (33,000) masahaba walikusanyika pamoja na wakakubaliana na kuhakikisha kwamba kila herufi imekaa pahali pake asili.

Kiarabu kimetofautiana kutamka baadhi ya matamshi ila maana ni ileile kwa kiswahili tunaita lahaja.

Ukhalifa wa Uthman ibn Affan ulikumbwa na hii hali watu walikuwa wakisoma Quran kwa kutofautiana matamshi kwa jinsi sehemu nyengine walivyoiandika kwa lahaja yao hususan watu wa Sham (ambapo kwa Zamani ilijumuisha Syria na Lebanon) na watu wa Iraq, Hudhaifa ibn Al Yaman ndiyo aliyompatia hii taarifa Uthman.

Khalifa Uthman alichukua copy ya mas-haf kutoka kwa Hafsa iliyoandikwa wakati wa Ukhalifa wa Aboubakr Siddiq kuitumia hiyo na kuigilizia yaani: Akaamrisha nakala nyengine ziandikwe chini ya uangalizi wa Zayd ibn Thaabit kutoka kwenye copy hizo na kuandikwa kwa kiarabu cha ki Quraysh.

Kisha ile aliyoitumia kunakili aliirudisha kwa Hafsa alipoichukua.

Kisha hizo nakala zikatumwa sehemu tofauti tofauti kwa magavana wa kiislamu na kisha kuamuru all the other Qur'anic material zichomwe moto na hiyo pekee ndiyo itumike kuhofia kuwa mbeleni kunaweza kukatokea ikhtilafu kubwa baina ya waislam.
 
Ukristo sio dini hata Qur'an ilisema wako wanao jita wakristo wengine wachamungu Qur'an imekusudia time zile bada ya kuondoka Yesu sio wote, ni wako walio amini Yesu si Mungu sio hawa wanao sema Ysu ni Mungu.



Ukristo sio dini ya Mungu ni dini ya Paulo.
 
Hoja yako haieleweki halafu ukristo hauwezi ukataka uhakikishwe na Uislam ukiokuja Karne ya 6 na kuenezwa na Mkureshi mmoja ambae hana maadili na utu katika kueneza dini yake
 
Unaleta utoto sasa hali ya kuwa watu wapo hapa kujifunza na kusahihisha yale yaliyoandikwa uongo.

Muhammad hapo awali alikuwa anaitwa nani?

Kwa sababu umesema awali alikuwa na jina tofauti na hilo!

Ili tuweke kumbukumbu sawa ni muhimu kuweka ushahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…