SoC03 Ukuaji wa technolojia kama chachu ya maendeleo kwa nchi za kiafika

SoC03 Ukuaji wa technolojia kama chachu ya maendeleo kwa nchi za kiafika

Stories of Change - 2023 Competition

Frank mtanganyika

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2018
Posts
497
Reaction score
785
Dunia inaenda kasi sana kwenye swala la maendeleo ya teknologia.
tumekuwa tukishuhudia ongezeko kubwa sana la uanzilishaji na uendelezaji wa teknologia, pamoja na kuwa maendeleo haya yameshuhudiwa zaidi kwa nchi za dunia ya kwanza pia sisi bara la afrika hatujaachwa mbali maendeleo haya yametufwata na kutufikia.

Hatuwezi kupingana na ukweli kuwa sisi pia tunapaswa kuwa katika mnyororo wa huu ufumbuzi mkubwa wa teknologia. Maana faida zinazotokana na teknologia na utandawazi ni nyingi na kama tunaishi katika hii dunia hatuwezi kupinga matumizi ya teknologia kwa kuwa maendeleo haya yanatuhusu moja kwa moja kwa maana yanarahisisha maisha kwa kuwa suluhu ya changamoto mbali mbali.

Kila jambo lina pande mbili kwa maana ya kwamba kuna upande wa mazuri na upande wamabaya, pamoja na faida nyingi zinazotokana na teknologia pia kuna sehemu ndogo ya adhari hasi zinazotokana na maendeleo haya ikiwemo uporomokaji wa maadili katika jamii ya kiafrika

Uzuri ni kuwa adhari hizi hasi zinaweza kuzuilika na tukabaki na faida tu ikiwa tutaamua tutumie utadawazi tuutawale na sio sisi ututawale kwa maana ya kuwa kama tutakuwa na mapokeo mazuri kwa kuelewa ni wapi tunataka huu utandawazi utukifikishe, tutaweza kuwa msaada mkubwa sana kwa kizazi kijacho.

Jamii yetu ni mfano wa mtoto anayekuwa, huwezi kumzuia kuchanganyika na watu lakini malezi bora ya mzazi ni pale anapomfanya mtoto aelewe huko nje kuna nini, kipi bora kwake na kipi anaweza kukitumia kwa namna gani ilikimfikishe mahali fulani ukweli ni kuwa atakutana na watu wa kila aina ila ukuaji mzuri wake utachangiwa pakubwa sana na uelewa wake kwa maana yapi mazuri, yapi mabaya na ayatumiaje hayo mazuri.

Huwezi kuupinga mfumo ukikataa kuendana nao basi mfumo utakutupa nje, tumeona namna maendeleo yanavyobadili mpaka maisha ya jamii yetu, hatuwezi kunga'ngana kutumia jembe la mkono kulima kwa karne ya 21 ilhali kuna vipawatila vidogo vinavyoweza kulima hekari zakutosha kwa garama nafuu na kwa mda mfupi

Nini kifanyike ili tuende sambamba na haya maendeleo?.

1. KUTUMIA VIZURI FURSA ZA UWEPO WA MIUNDOMBINU WEZESHI KATIKA TECHNOLOGIA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZO IZUNGUKA JAMII YETU.

Kuna kauli iliwali kusemwa na muasisi wa microsoft bill gates alisema. " Kuzaliwa masikini siyo kosa lako, ila kufa masikini ni ujinga wako". tunaishi kwenye karne ambayo fursa zipo kiganjani mwetu zimetuzunguka karbu sana kuliko tunavyofikiria

Uwepo wa miundombinu wezeshi kama huduma ya intaneti na upatinaji mrahisi wa simu janja, taraklishi n.k ni moja ya nyezo za kuchochea sana maendeleo kwa kutatua changamoto zinazotuzungusha. Ukweli usiopingika tena teknologia inayovumbuliwa kwetu ina uwezo wa kusambaa sana na kutumika kwa urahisi kwa sababu inakuwa imezingatia mazingira ya jamii yetu.

Tunaona kunavyokuwa na changamoto ya soko la ajira kwa vijana wengi kuhitimu vyuo na kukosa kazi ila ukweli ni kuwa kuna kazi ambazo ziko mtandaoni ambapo kijana mwenye uwezo wa kupata simu janja ya bei ndogo kabisa( ambapo wengi wanazo) na kuwa na huduma ya inteneti anaweza kufanya kazi ya kampuni iliyoko antanario canada ikiwa yeye yuko kijijini kwake nanjirinji mtwara, uzuri hata ujuzi na uzoefu unaotakiwa bado kuna nafasi ya kujifunza kupitia mitandao mbali mbali

Leo hii tunaona kuna programu nyingi za simu na mifumo ya kielekroniki inayoanzishwa kwa lengo la kutatua changamoto flani katika jamii. Kinachosikitisha hizi programu nyingi sio za wazawa sio kwamba tumeshindwa kuunda za kwetu lah. Ni utayari tu na udhubutu kwa maana tuna nafasi ya kuendelea zaidi kwa ufumbuzi unaotoka katika jamii yetu kwakua sisi tunauwelewa wa mazingira yetu zaidi kukiko yeyote yule. Na uzuri ni kuwa upatikanaji wa elimu na uzoefu umerahisishwa tunaweza kujifunza wenzetu wanafanya nini tukaja na suluhisho linaloendana na mazingira yetu. Uwepo wa mifumo inayorahisisha uundaji wa programu ni njia rahisi tunaweza kutumia.


2. MCHANGO MKUBWA WA SEREKALI NA WADAU MBALIMBALI KUCHOCHEA MAENDELEO YA SAYANSI NA TEKNOLOGIA

nafasi ya serekali ni kubwa sana kwa kuweka mazingira wezeshi na kuwa na sera zinazorahisisha ukuaji wa teknologia. Mfano; tunaona jinsi huduma ya intaneti inavyokuwa kwa sasa duniani na kwa sasa ni moja ya mahitaji ya msingi, Je ni upi mchango wa serekali kuona huduma hii sasa ni hitaji la msingi kwa mwanadamu kama ilivyo chakula, malazi na mavazi?. Usaambaaji wa huduma ya intaneti mpaka umefika mpaka vijijini?. huduma ikiwepo kwa wingi na kwa urahisi garama zake zitakuwa za chini, serekali inatakiwa ikaribishe wawekezaji mbalimbali kwa kufanya mazingira yawe rafiki kwa kuwa na sera rafiki zitakazo ruhusu mashirika na kampuni zipendezwe kutoa huduma ya intaneti na nchi yetu iwe inahuduma mpaka vijijini hii itasaidia kuwa na ubunifu utakao tokana na teknologia leo hii hakutakuwa na shida ya mkulima kuumiza kichwa wapi auze mazao yake au kwa mamna gani anaweza kukwepa walanguzi badala yake gunduzi zitakuwepo nyingi za kurahisisha maisha kwa watu wa hali ya chini.

Wadau wa teknologia ikiwemo taasisi zinazojishuhulisha kutambua na kuongoza huduma mbalimbali zinaweza kuongeza mchango wao kwa kuwezesha na kufadhili zaidi guduzi mbalimbali zinazolenga kurahisha huduma ya kiteknologia. Mabenki yanaweza kutumia kufadhili mikopo ya gunduzi za kiteknologia zinazolenga kutatua changamoto zinazozunguka jamii. Hii itafanya hata vijana wanao maliza elimu yao ya chuo wao na mtizamo chanya kuwa ni kitu gani wanaweza kufanya kwa jamii yao kitakachokuwa chachu ya maendeleo kwa maana wanajua wadau wako watakaoweza kufadhili gunduzi zao, uwepo wa mifumo tambuzi itakayosimamia watu wenye gunduzi zao kwa kuwafadhili kwa kuwaongezea elimu, kuwawszesha na vifaa n.k
hii itajenga mtizamo wa kizendo kwa jamii.

Nipende kunukuu kauli ya Baba wetu wa taifa hayati mwalimu jukius nyerere aliwahi kusema " maendeleo hayanabudi yawe na uhusiano na maisha ya watu hayanabudi tuyapime yamefanya nini kwa watu". Tunajua ziko taasisi zinazoshughulikia ukuaji wa teknologia kwa mahusiano na maendeleo Je!?. Tumepima kweli zina gusa maisha ya watu moja kwa moja?.upi mchango wao katika kuendeleza technologia ipatikane kirahisi na kufikia watu wengi zaidi?. Inapasa tujitadhimini na inapobidi tukubali kubadilika kuendana na nini hali ya maisha inataka kwa sasa.

ASANTE!.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom