Ukubwa au ukongwe wa Simba na Yanga ni upi?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Sijawahi kuelewa ukubwa wa hizi timu mbili za Simba na Yanga, Hivi timu kubwa zenye miaka 90 zinashindwaje kujenga uwanja hata mdogo Tanzania yenye ardhi kubwa na gharama ndogo za ujenzi?! Au umasikini wa watanzania unatafsiriwa kwenye hizi timu pia?

Huwa nasikia watu wanaziita timu kubwa au kongwe lakini siwelewi wanamaanisha nini, au huo ukubwa/ ukongwe wanaomaanisha ni wingi wa mashabiki na watu maarufu walio wanachama wa hizi timu wanaopigana vijembe?

It doesn't make any sense.
 
Kwahiyo kuwa na uwanja ndio zinakua timu kubwa?
 
Kuna wazee wengi tu mjini wamekufa bila kujenga nyumba
 
Uwanja ni nembo na prestige ya timu ya mpira, hakuna timu kubwa duniani za maana zisizo na uwanja wake
 
Kuna wazee wengi tu mjini wamekufa bila kujenga nyumba
Mimi naongelea "TIMU" ambayo ni Taasisi, yenye miaka 90 na ambayo haitegemewi kufa siku moja.
 
Mbona Unaijumuisha na Simba...!

Simba tayari Wanao Uwanja Boko na Wanautumia Kwa Mazoezi. Kilichobakia ni Kuuboresha tu ili Mechi za Ushindani Zipigwe hapo..!

Wee kama sio Utopolo Komaa na Yanga mpaka Wakujibu Wana Ukongwe Gani Wakati kiwanja hawana .?
 
Uwanja wa Simba unachukua mashabiki wangapi?
 
N wamejua kuteka akili za watu hasa wasio na akili timamu.
 
Sijawahi kuelewa ukubwa wa hizi timu mbili za Simba na Yanga, Hivi timu kubwa zenye miaka 90 zinashindwaje kujenga uwanja hata mdogo Tanzania yenye ardhi kubwa na gharama ndogo za ujenzi?! Au umasikini wa watanzania unatafsiriwa kwenye hizi timu pia?

Huwa nasikia watu wanaziita timu kubwa au kongwe lakini siwelewi wanamaanisha nini, au huo ukubwa/ ukongwe wanaomaanisha ni wingi wa mashabiki na watu maarufu walio wanachama wa hizi timu wanaopigana vijembe?

It doesn't make any sense.
Mbona hilo jambo la kawaida kwenye medani ya mpira wa miguu kuna timu nyingi maarufu duniani tena zenye mashabiki na mafanikio makubwa kuliko hizo timu mbili za kariakoo hazina uwanja binafsi kuzitaja kwa uchache ni chelsea, man city, inter milan na ac milan
 
Hizi timu ni kongwe kwa sababu Zina miaka zaidi ya 75 kiumri Ila hazina ukubwa wowote Kama timu za juzijuzi Kama Mazembe na Mamelod Wana vikombe vya Africa na timu Kama Jkt, Kmc na Azam wanamiliki viwanja Simba na yanga sio timu kubwa.
 
Back
Top Bottom