Ukubwa wa GPA si kuwa na maarifa.

Nkaka

Senior Member
Joined
Apr 7, 2014
Posts
108
Reaction score
16
Wanajamvi nimekuwa nikihoji kigezo cha GPA kuwa sifa yakufundisha chuo kikuu ila kwautafti wangu kuna watu wanafirst class zisizoendana na wanachokjua
 
Kizazi kipya. napenda utambue kuwa chuo kikuu hakiandai walimu wa chuo kikuu ( na hili ndio tatizo). Whether mtu anavitu kichwani au hana inategemea kama umempa Paper akashindwa au ume interview naye akashindwa au umefanya vyote. Sasa inawezekana kabisa mtu akawa na first class na akashindwa kabisa kuwa na confifdence ya mwl wa chuo kikuu wakati yule mwenye GPA 2.8 akawa fit sana kuelezea ishu, hivi ni vipaji tofauti. Ni ujinga sana kufikiri kwamba mtu akiwa na GPA kubwa atakuwa mzuri kwenye kufundisha chuo kikuu. wengine hawapaswi kufundisha bali wafanye tu kazi za utafiti nk huko wanaweza kuwa wazuri zaidi. hali halisi ilivyo sasa watu wanaingia kufundisha vyuo vikuu kama ajira kwanza lakini pili kwa sababu wana qualifications za kitaaluma,. Msingi huu si sahihi na ninakuunga mkono Mdau kwa kuona hili.
Sisera.
Wanajamvi nimekuwa nikihoji kigezo cha GPA kuwa sifa yakufundisha chuo kikuu ila kwautafti wangu kuna watu wanafirst class zisizoendana na wanachokjua
 
the issue ni vice versa kibongo bongo..... komaa wiki mbili kabla ya mtihani....kutana na mtihani mule mule ulimokariri tusua mambo mengine juu kwa juu
 
Mtizamo wangu sasa kigezo kwamba ili ufundishe chuo kikuu lazma degree yakwanza uwe na upper2nd class au kuwa tutorial uwe na 3.8 si ishu tena nashauri kigezo kiondolewe
 
Kunapokuwa na uhitaji wapokee mambi na kila mt apewe fursa ya kutetea ufaulu otherwise hki ndicho chanzo cha rushwa ya uroda kwa dada zetu vyuo ili kupewa paper
 
ingetafutwa njia nzur sababu rushwa na ngono ndio zinazotawala vyuoni ili mtu awez kupata gpa nzuri na hata mwisho wa siku aweze kubakishwa kwa kigezo cha gpa hali halisi hana uwezo hata wa kukopia nalaani san hasa haya ma vyuo ya private coz wanajifanya wanabana elimu yao kwa kupandisha grade za ufaulu mwisho wa siku wanafunz wanamaliz na gpa mbovu then wanajisifia eti elimu yao no bora hali ya kuwa ktk interview wanaangalia ufaulu
 
Kua na GPA kubwa haimaanishi kua mwanafunzi ana uwezo mkubwa darasani zaidi ya wenzake.Kuna rafki yangu yeye alkua akiingia kwenye chumba cha mtihani na smartphone yenye nots zote,ananakili kila kigum kwake na mwisho wa siku GPA kubwa lakini kichwani hamna kitu.
 
Mtizamo wangu sasa kigezo kwamba ili ufundishe chuo kikuu lazma degree yakwanza uwe na upper2nd class au kuwa tutorial uwe na 3.8 si ishu tena nashauri kigezo kiondolewe

Wakati wewe unawaza kiondolewe, wenzio wana mchakato wa kupitisha hiyo GPA ndio iwe kigezo cha kwanza kwa vyuo vyote. Kwa sasa Mzumbe ni. 3.5 wkt UDSM ni 3.8

Na kwa vyuo kama UDSM, kwa sasa hakuna kubakizwa, nafasi za kazi zikitoka unaomba, ukiwa shortlisted utaitwa kwenye interview, ukishindwa hata kama una first class unaachwa.

Na kigezo kikishushwa, wengine watakuja hapa na kusema "siku hizi hata vilaza wanakuwa walimu wa chuo kikuu"
 


Hahaha iko njema ukiwa na bahati ya kuotea mtihani!
 
Wasipoangalia sikumoja watajikuta wamejisahau na kuanza kuomba wapewe Rais na Waziri Mkuu toka nje ya nchi!!!

Nenda chuo chochote kizuri duniani utakuta huo ndio utaratibu.nimefanya masters yangu uk at coventry university. Hiki ni chuo ni miongoni mwa vyuo vikubwa duniani.nao pia uchukua watu wenye ufauru wa juu kuwa wakufunzi.nenda Harvard, Oxford, Yale University, university of cape town nk..wote wanatumia huo utaratibu.sasa labda ww anzisha chuo tuone km utataka watu wa lower second na pass ndio wawe waalimi. Nakubali kuwa wapo watu wana lower class na hata pass japo wapo vizuri. Lakini tukumbuke kuwa the end does not justify the means. Km huyo mtu anajua madema ilibidi aoneshe hata kwenye vyeti vyake kuwa yuko vizuri.
 
Hahaha mtu akiwa na bahati ya kuotea mtihani ndo anayedaiwa kuwa kipanga tena!

Unaweza kuotea mtihani wa kidato cha nne au sita lakini km ujuavyo kuwa matokeo ya mtu ya chuo ni wastani wa kila alichopata kuanzia mwakawa kwanza hadi wa mwisho. Sasa hapo kubahatisha kunatoka wapi?
 
Unaweza kuotea mtihani wa kidato cha nne au sita lakini km ujuavyo kuwa matokeo ya mtu ya chuo ni wastani wa kila alichopata kuanzia mwakawa kwanza hadi wa mwisho. Sasa hapo kubahatisha kunatoka wapi?

Unadhani wanalijua hilo!!! kuna wengine wapo chuo lkn bado hawajielewi. Badala ya kukomaa na shule na kujiwekea malengo, wanakuja kulalama mitandaoni.
 
Hahaha mtu akiwa na bahati ya kuotea mtihani ndo anayedaiwa kuwa kipanga tena!

First yr mtu kasoma kozi 12, second yr, kozi 11, third yr kozi 12, na GPA ni above 3.8, unajua GPA inavyokokotolewa? hakuna ukipanga hapo wala kubahatisha! It's all about determination. Otherwise awe mtu wa chabo, na ipo siku atakwama. (ninao mfano hai). Alipata GPA kubwa undergraduate, ilikuwa wkt ule mwenye GPA kubwa anabakizwa bila hata usaili, akapelekwa kusoma MA, chabo zikawa ngumu, alishindwa kufikisha vigezo, na kazi akatimuliwa.
 
Wanajamvi nimekuwa nikihoji kigezo cha GPA kuwa sifa yakufundisha chuo kikuu ila kwautafti wangu kuna watu wanafirst class zisizoendana na wanachokjua

So unataka wenye gpa ndogo ndio wafundishe? Yaan unataka ukawafundishe watu masomo ambayo hata ww mwenyewe ulikuwa unapata makalai!
 
Mtizamo wangu sasa kigezo kwamba ili ufundishe chuo kikuu lazma degree yakwanza uwe na upper2nd class au kuwa tutorial uwe na 3.8 si ishu tena nashauri kigezo kiondolewe
kwahiyo wewe unataka mtu mwenye GPA 2.1 akafundishe chuo kikuu?. kitu cha kwanza kabisa kitakacho kusaidia kujua mtu anauwezo wa kufundisha ni GPA kubwa.kinachofuata ni kuwachuja wenye GPA kubwa,si wote wenye GPA kubwa wanakuwa T.A, AU lecturers.
pili twende turudi mwenye GPA kubwa hata kama alipitia madesa tu ni rahisi ku change na kuadopt mazingira na kuwa na uwezo wa kufanya vitu tofauti... wenye GPA kubwa 80% wanauwezo wa ku kufundisha chuo kikuu.asilimia 30 ya wenye GPA ndogo ndio wanauwezo wa kufundisha chuo kikuu kwa mtazamo wangu.
tatu ubaya zaidi nashangaa mnatetea kitu ambacho kipo wazi mfano"waliofaulu kidato cha nne kwa kiwango cha chini ndio wanaokwenda kusomea ualimu na kuwa waalimu,na wanaotoka form 6 secondary na advance pia ALAFU TUNALALAMIKA KWAMBA SELIKALI INACHUKUA WATU WENYE UWEZO MDOGO KWENDA KUFUNDISHA WANAFUNZI.JE NA ELIMU YA JUU WALIOFAULU KWA KIWANGO CHA CHINI WAKAWAFUNDISHE WATU WANAOANDALIWA KUWA WATAALAMU KWENYE SECTA TOFAUTI TOFAUTI?
 
the issue ni vice versa kibongo bongo..... Komaa wiki mbili kabla ya mtihani....kutana na mtihani mule mule ulimokariri tusua mambo mengine juu kwa juu
hapo sasa inakuwa ishu.first class ninazozitetea hapa ni zile cream ,yaani wanaojua mambo kwa undani na kusoma ili kupata ujuzi si kufaulu peke yake
 
safi kabisa nakupa like 1000 mkuu.wakisema wachukue lecturer mwenye gpa yeyote basi kila mtu angekuwa anataka awe lecturer na thamani itashuka sasa maana watasema sikuhizi hadi vilaza lecturers.....
 
hahaha mtu akiwa na bahati ya kuotea mtihani ndo anayedaiwa kuwa kipanga tena!

necta ndio tulikuwa tunaiotea labda.maana masomo ya miaka minne unapimwa kwa masaa matatu.
Sasa ili uwe na first class inabidi uwe na a's na b+ za kutosha tangu mwaka wa kwanza hadi wa mwisho,sasa mtu anaotea vipi kuanzia mtiani wa kwanza hadi wa mwisho?na siku hizi first class si nyingi kwa upande wa utafiti wangu kwa vyuo kama vitano nilivyopita graduation zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…