Ukulima wa shayiri(katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro)

sixty nine69

Member
Joined
Jul 30, 2014
Posts
66
Reaction score
14
Shayiri nijamii flan iv ya ngano ambayo hutumika sana kutengenezea Pombe, zao hili lina uhitaji mkubwa sana apa nchini kwetu hasa kwa viwanda vya bia kama vile TBL and SBL, naomba mwenye uzoefu katika hili atupe taarifa kutokana na maswali yafuatayo

1.Jins linavyo limwa
2.Gharama zake za kulimia,na kuuza pia
3.Na upatikanaji wa ardhi ya kulimia hasa katika mikoa niliyo itaja

Naomba kuwasilisha mada

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mkuu shairi inalimwa baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, na Manyara, Kwa Arusha inalimwa Wilaya za Karatu, na Monduli. Mkoa wa Manyara nazani inalimwa Hanangi tu, na Kilimanjaro inalimwa eneo linalo itwa West Kilimanjaro, hapa ndo kwenye mashamba makubwa kabisa ya hii ngano Tanzania nzima, make kuna makaburu pale na wanavifaa si mchezo.

Tatizo ni kwamba Shairi nikwamba wanunuzi ni wawili au unakuta ni mmoja tu TBL, ingawa ina kazi nyingi sana zaidi ya hizo za Bia.

Kupata aridhi ya kulima hii kitu sio kazi ndogo kwa sababu inalimwa baadhi tu ya maeneo mfano KARATU utakuta inalimwa baadhi ya maeneo sio wilaya nzima, hivyo hivyo Manyara na hivyo hivyo Kilimanjaro, Mfano Kilimanjaro nzima shairi inalimwa west kilimajaro pekee. Na KARATU nzima utakuta maeneo yanayo limwa ni maeneo ysio zidi ma nne.
 
Asante sana bwana chacha mm ni mgeni katika hili jukwaa na kati ya watu wote nime ya kubali sana mawazo yako katika post mbali mbali!

Mbali na apo kutokana na ulicho kiandika so una nishaurije apo, niendelee kutafuta posibility ya kupata iyo ardhi au ni angaike tu na mzao mengine.

Maana mm nilisha wahi kufanya field TBL na nika ambiwa iyo ngano/shairi huwa haitoshi mpaka wana amua kuagiza toka nje ya nchi, thus why nikaona nitafute possibility ya kuweza kulilima ilo zao.
 

Unaweza tafuta aridhi mikoa mingine mkuu kwa sababu hata Iringa inalimwa, na Sumbawanga kama sikosei, inapenda sana sehemu za Baridi so jaribu maeneo yenye baridi kari hapo unaweza pata shamba ila kwa mikoa ya Arusha, kilimanjaro na Manyara ni vigumu sana labda ya kukodisha ila ya kutosha kabisa kilimo kikubwa hayapo. ni kweli huwa haitoshelezoi na wanaagiza kutoka South Africa au hata huko URUSI ambako ndo ipo ya nyingi
 
Ok asante sana bwana chasha,
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu nasomea Agriculture Engineering thus Y nilikuwa naulizia ilo zao, nimeipenda sana post yako katika kilimo cha mpunga ambayo umeshauri wa TZ wengi waachane na biashara za ku copy hasa ya kununua mpunga na kuficha wakitegemea kuuza kipind bei zime panda wakti wakenya wana waza ku grade.
Kweli wa Tanzania tunahitaji kubadilika katika hili. Keep it up Chacha Idea zako zitatufikisha mahala pazuri

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Katika taarifa ya habari ya wiki iliyopita(juma5 au alhamisi, sikumbuki vizuri) kupitia TeleVishen ya StarTV, TBL wametangaza kuwa wataanza kutoa mbegu za shayiri kwa wale wote wanaolima hilo zao, kwa taarifa zaidi waweza tembelea kiwanda cha TBL kilichokaribu nawe.
 
ktk taarifa ya habari ya wiki iliyopita(juma5 au alhamisi, sikumbuki vizuri) kupitia TeleVishen ya StarTV, TBL wametangaza kuwa wataanza kutoa mbegu za shayiri kwa wale wote wanaolima hilo zao, kwa taarifa zaidi waweza tembelea kiwanda cha TBL kilichokaribu nawe.
 

Si kutoa huwa tiyari wanatoa mbegu tangu siku nyingi, Ila ukweli unabakia kwamba shairi inalimwa baadhi ya maeneo na si kila eneo unaweza lima si kama mahindi, That is why hata Mikoa inayo lima utakuta ni sehemu ndogo sana inakubali ngano. na wao siku zote huwa wanatoa mbegu ila si kwamba wanagawia kila mtu no wanagawia wakulima wanao lima na kuna utaratibu huwa wanatumia
 

asante kiongozi!
 
Bwana chasha vp ww ulisha wahi kujaribu kulima zao hilo?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 

Habari kiongozi.
Nisingependa kukukatisha tamaa katika hili, mimi ntajikita point number mbili kwenye gharama za kuudumia shamba na kuuza.
Gharama za kukodi shamba kwa west klmkwa heka moja tsh 45,000
kulima kwa jembe la trekta 40,000
kurudia na haro 40,000
kupanda kwa planter 30,000
mbegu sikumbuki vizuri but 50,000
mbolea yakupandia 45,000
dawa za kutu 60,0000
Dawa ya majani 18,000 mpka 30,000
dawa ya kuuwa kimamba yakichina 18,000
kuvuna 40,000 kwa heka.
kuna kushona magunia baada ya kuvuna kila gunia 500
kupakia kwenye gari kwa ajili yakusafirisha 1000
kukodi usafiri ili upeleke kwenye godown lao NMC Arusha kutoka west 300,000
kuwaonga matrafiki barabarani andaa 50,000
garama zako za kula, simu, usafiri, kuwalipa wasimamiz utajiju.
jumla kwa heka moja unaweza tumia kama laki tano hivi.

Kwa heka moja mwaka huu wakulima wengi nikiwemo na mimi tumepata wastan wa gunia nne.

Kila gunia lina wastan wa kilo 100,
Majamaa wananunua kilo moja tsh kuanzia 720 mpaka mia 900.
Kwahiyo inategemea na ubora. Unaweza peleka shairi nzuri wakakuambia haina ubora yamewakuta wengi
wastan wa heka utapata 80,000x4=320,000
Wakati huo wewe umetumia zaid ya laki tano.

Ni mchezomchafu jamaa wanawafilisi wakulima sana na ndo maana wenyewe hawalimi wanajua nn wanachokifanya kwa wakulima.
In shoti ni weziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Kule china wangenyongwa
 
Kabla ya kuanza tembelea wakulima wa karatu, monduli, west klm na basutu.
Kwa ushauri wangu lima ngano au mtama mwekundu kidogo wanunuzi ni wengi tofauti na shairi, usipowauzia serenget utawauzia tbl. Halafu isitoshe unaweza ambiwa shairi yako ni chakula cha nguruwe haina ubora kamwage
 

Ni mtama mweupe au mwekundu? Ninavyo jua ni mtama mweupe na si mweipe bali kuna aina ya mbegu.
 
Asante sana sana bwana makaptula pamoja na chasha, yani jamaa wa TBL na serengeti wanavyo wa convince wakulima kulima utadhani kila kitu kinaenda sawa, Now nimeisha jua kwann watu wengi hawa jihusishi na hiki kilimo

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 

Mkuu ila Bado kwa kilimo chetu ni lazima jamaa wanunue shairi kutoka nje, haitoshelezi kamwe,
 
Lakini jaman tusihishie kula umutu, bwana chasha pamoja na makaptula nyie mnaona nn kifanyike ambocho kitawapa mafanikio ili mradi watu wanao jihusisha na wanao taka kujihusisha wanufaike na kilimo ichii

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 

Mkuu ila hii ngano ina matumizi mengine sema watu hawajajua ila inaweza kuwa na soko zuri kuliko la bia, mi mwemyewe nahitaji gunia 20 za shairi
 
Chash kwan ngano hii tunayo izungumzia, na bharesa anatumia iyo iyo?

Alafu chasha ningependa sikumoja nitembelee poutry farm yako kama inawezekana ni PM namba yako na wapi unapatikana

Sent from my BlackBerry Bold 9780 using JamiiForums
 
 
kilimo cha shairi inataka umakini,tyming ya mda,vifaa bm tractor zako mwenyewe ikiwezekana na mashne yakuvunia ngano yakwako mwenyewe hapo unaweza ukafanikisha kilimo chake.kilimo hiki kinalipa ukilima km large scale ndyo inalipa.wapo wabongo wanaolima maelfu ya ekari ya shairi,ila wanavifaa vyao wenyewe km combine harvestar na matrekta na wanamudu kilimo bila tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…