Shayiri nijamii flan iv ya ngano ambayo hutumika sana kutengenezea Pombe, zao hili lina uhitaji mkubwa sana apa nchini kwetu hasa kwa viwanda vya bia kama vile TBL and SBL, naomba mwenye uzoefu katika hili atupe taarifa kutokana na maswali yafuatayo
1.Jins linavyo limwa
2.Gharama zake za kulimia,na kuuza pia
3.Na upatikanaji wa ardhi ya kulimia hasa katika mikoa niliyo itaja
Naomba kuwasilisha mada
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Habari kiongozi.
Nisingependa kukukatisha tamaa katika hili, mimi ntajikita point number mbili kwenye gharama za kuudumia shamba na kuuza.
Gharama za kukodi shamba kwa west klmkwa heka moja tsh 45,000
kulima kwa jembe la trekta 40,000
kurudia na haro 40,000
kupanda kwa planter 30,000
mbegu sikumbuki vizuri but 50,000
mbolea yakupandia 45,000
dawa za kutu 60,0000
Dawa ya majani 18,000 mpka 30,000
dawa ya kuuwa kimamba yakichina 18,000
kuvuna 40,000 kwa heka.
kuna kushona magunia baada ya kuvuna kila gunia 500
kupakia kwenye gari kwa ajili yakusafirisha 1000
kukodi usafiri ili upeleke kwenye godown lao NMC Arusha kutoka west 300,000
kuwaonga matrafiki barabarani andaa 50,000
garama zako za kula, simu, usafiri, kuwalipa wasimamiz utajiju.
jumla kwa heka moja unaweza tumia kama laki tano hivi.
Kwa heka moja mwaka huu wakulima wengi nikiwemo na mimi tumepata wastan wa gunia nne.
Kila gunia lina wastan wa kilo 100,
Majamaa wananunua kilo moja tsh kuanzia 720 mpaka mia 900.
Kwahiyo inategemea na ubora. Unaweza peleka shairi nzuri wakakuambia haina ubora yamewakuta wengi
wastan wa heka utapata 80,000x4=320,000
Wakati huo wewe umetumia zaid ya laki tano.
Ni mchezomchafu jamaa wanawafilisi wakulima sana na ndo maana wenyewe hawalimi wanajua nn wanachokifanya kwa wakulima.
In shoti ni weziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Kule china wangenyongwa