Ukumbi wa Mlimani City utalipuka kwa shangwe baada ya Lissu kutangazwa mshindi katika kinyang'anyiro cha kumchagua mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA

Ukumbi wa Mlimani City utalipuka kwa shangwe baada ya Lissu kutangazwa mshindi katika kinyang'anyiro cha kumchagua mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Binafsi,kwa asilimia 95 , naamini Lissu atapata kura nyingi kuwazidi waitia nia wengine wanaowania kuteuliwa na chama kupeperusha bendera ya CHADEMA kwa nafasi ya uraisi ,na hili litadhihirika pale matokeo ya kura yatakapotangazwa.

Siku hiyo natarajia ukumbi utalipuka kwa shangwe na vigelegele ambavyo havitaishia tu ndani ya ukumbi bali shamrashamra hizo zitaendelea nje ya ukumbi na baadae kuhami mitandaoni.

Media za kimataifa nazo hazitakuwa nyuma katika kutangaza matokeo hayo huku Lissu akihojiwa aseme machache juu ya ushindi wake bila kusahau Mbowe kama mwenyekiti kwani ni lazima watataka maoni yake.

Ikitokea hiyo asilimia 5 ndio itatoa mshindi kwa maana ya Nyalandu,ukumbi utapoa ingawa wapo wachache watashangilia ila CCM ndio wataongoza kupokea kwa furaha matokeo hayo kuliko wana-CHADEMA wenyewe.

Kama ambavyo nimekuwa nikisema humu mara kadhaa,Lissu anabebwa na nyakati kwani hizi ni nyakati zake kama tusemavyo: "kila jambo na wakati wake" na wakati huu ni wa Lissu.


Tusubiri.
 
Kama Mbowe ataruhusu demokrasia ndani ya chama na kwa wajumbe bila shaka Tundu Antipas Lissu anakwenda kushinda.

Ila kama atafanya biashara kama miaka mitano iliyopita basi Lazaro Nyarandu ndie mshindi.
Full Stop!
 
Huo ndio ukweli mkuu.

Wajumbe wasijewakafanya makosa.

Nyalandu ilikua tu km backup iwapo lolote lingetokea kwa Lissu either kuahirisha kuja nchini akihofia usalama wake ama kuuwawa na kina musiba pindi akitua nchini.

Lkn Mungu aliyelitendea miujiza taifa kupitia kwa Lissu amewapooza madikteta Lissu amerudi kuungana na watz kutafuta ukombozi wa taifa
 
Image
 
Back
Top Bottom