Ukungu wawa tishio Njombe, TMA wawaonya madereva

Ukungu wawa tishio Njombe, TMA wawaonya madereva

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa ufafanuzi kuhusu hali ya mawingu na ukungu unaoamb.jpg

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa ufafanuzi kuhusu hali ya mawingu na ukungu unaoambatana na manyunyu katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Njombe.Imesema hali hiyo imepunguza uono na kusababisha baadhi ya madereva kuwasha taa za magari ili kuona mbele.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Septemba 16, 2026, Meneja wa TMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Elias Lipiki amekiri kuwepo kwa mawingu na ukungu mzito katika maeneo ya Mkoa wa Njombe, akisema hali hiyo pia imeonekana katika maeneo mengi ya mashariki mwa nchi.

Amesema kwa kuwa Njombe ni sehemu ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, miinuko iliyopo katika maeneo hayo hufanya hali hiyo iwe rahisi kujitokeza, huku katika baadhi ya maeneo mawingu yakigusa ardhi na kusababisha ukungu.“Sasa katika maeneo yaliyopo juu sana, unyevunyevu huu huganda na kutengeneza matone madogo madogo, kinachoitwa mawingu, lakini yakitokea karibu na ardhi au kugusa ardhi tunaita ukungu,” amesema Lipiki.Soma zaidi kwenye tovuti ya Mwananchi
 
Mbona siku zote Masika njombe huwa ni hivyo hivyo,
 
Back
Top Bottom