Ukusanyaji wa kodi ya ongezeko la thamani, vat

SAMMYT

Member
Joined
Jul 3, 2011
Posts
22
Reaction score
6
Wana JF naomba mnisaidie jambo moja. Hivi kujisajili kwa ajili ya kulipa VAT ni option? au Mandatory? maana ninachoshangaa wanotaka kusajiliwa kwa ajili ya kulipa VAT wanazungushwa sana wakati wanauza bidhaa ambazo zinalipiwa VAT?

Na pia kwa uzoefu wangu wauza mafuta ya diesel na pertol haiingii akilini kuwa hawaezi kuuza milioni ishirini kwa mwaka lakini inaonesha zaidi ya asilimia 90 ya hao wafanya biashara hawalipi VAT maana ukiangalia stakbadhi wanazotoa haioneshi kuwa wamesajiliwa na VAT.

Sasa kwa nini serikali ing'ang'anie kuwatoza kodi PAYE wafanyakazi wakati hawa wenye vituo vya mafuta wamekusanya kodi halafu hawaifikishi TRA? au hii ni biashara ya watu wa TRA? Naombeni msaaada wa mawazo
 
Naona nusu ya mapato huenda serikalini na nusu huenda kwa matumbo ya watu.
Ndo maana wafanyakazi wengi wa TRA hawashikiki mtaani wana mijihera.
Kuna mmoja ninamfahamu kajenga hotel ya ghorofa sita ukiidhaminisha amespend sio chini ya 4billion
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…