Ukwaju! Ukwaju

kalikumutima

Senior Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
147
Reaction score
46
Naleta kwenu wazo la biashara.Naomba mtu ambae anaweza akapata soko la uhakika la ukwaju wa asili tufanye kitu cha maana kuna sehemu nimepita nimekuta upo wa kutosha.

Nikajiuliza akina Azam wanapiga hela kwa ukwaju wa kuweka flavour tu,je kikiwa kitu asilia?!karibu kwa kuboresha wazo langu
 
Kilo shilingi ngapi???
 
Mkuu kuna kitu haujakielewa... Costs of Products kwenye Free Market... Azam atachouza yeye hapo huenda faida yake kwenye kila Tshs. 500 isifike hata senti hamsini

Kuna costs za production
Packaging
Promotion
n.k.

Wewe ukisema utengeneze kitu fresh kuna mambo kama shelf life na itabidi uuze at a premium price na ufanye marketing ya nguvu.., unachoweza kufanya ni kuangalia niche market (watu wachache waliokuzunguka kuwauzia fresh juice at a premium price).., na vyuma hivi vilivyokaza wapo wa kutosha..

Cha maana tafuta soko la nje watu wanaoweza kulipa premium price
 
Nikimpata anaetengeneza ili akaniambia kilo moja anatoa glass ngapi ingependeza zaidi.

Maeneo ambapo nimeona ukwaju mwingi wanauza kwa mafungu hivyo ninampango nikikamilisha kazi iliyonileta huku nichukue mafungu kadhaa nikayapime ili nijue kilo moja ni mafungu mangapi na kwa huku itakuwa imecost kiasi gani.
 
Mimi natengeneza lambalamba za ukwaju. Kilo moja sikosi 8000-10000 kama faida
 
Sio kweli tuwaze kufanya local packaging pia local market kwanza, simple mnapiga pesa
 
Sio kweli tuwaze kufanya local packaging pia local market kwanza, simple mnapiga pesa
Local packaging ni nini ni bure ? au unamaanisha kuuza barafu zile za mashule.., packaging means cost and cost means higher prices..., watu kama kina Azam wanaweza kuchaji pesa ndogo sababu wanauza volume kubwa..,

Wewe inabidi uuze premium price hata ukiuza quantity (volume ndogo) bado upate faida..,
 
Ninanunua kila week kilo 40 kuna mmoja ananiuzia kilo 1,000 mwinginr kilo 900.
So ukishauleta tutawasiliana ila bei zangu ni hizo nazochukulia, pungufu ya kilp 40 kilo moja moja wanauza 1,500 mpaka 2,000
 
Ninanunua kila week kilo 40 kuna mmoja ananiuzia kilo 1,000 mwinginr kilo 900.
So ukishauleta tutawasiliana ila bei zangu ni hizo nazochukulia, pungufu ya kilp 40 kilo moja moja wanauza 1,500 mpaka 2,000
Unatengenezea Juice,ice cream au wauza rejareja?
 

Mbona azam ananunua
Peleka kwake
 
mkuu
ulifanikiwa kupata soko la ukwaju?
 
Ukwaju ni mkali balaa. Kilo moja usiulizie glass uliza lita ngapi..... Mimi nilishatengeneza home ukwaji nusu kilo baada ya kuloweka na kuuchuja nikatoa ndoo ndogo moja..... Na bado ulikuwa mkali ilitakiwa niudilute na nusu ndoo nyingine....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…