deci na forever living ni vitu tofauti, moja wanagawa pesa bure, nyingine unakuwa machinga wa kuuza bidhaa kwa kamisheni!
Kwa jicho la haraka haraka DECI na FL ni tofauti lakini ili kupoteza maana halisi ya Pyramid scheme ndio wameingiza bidhaa ndani yake
Inabidi kwanza kujua nini maana ya Pyramid Scheme ndio utaelewa logic nzima ya hawa jamaa...this is a win lose situation
Hao unao waona wanadai wamekua na mafanikio hawauzi tena bidhaa maana chaneli zao zimekaa vizuri wamejiunga siku nyingi, balaa liko kwako unaetoa laki saba na nusu leo
In short this people they dont sell product as you may think, the use product to get more people to join in network
Faida hawapati kwa kutegemea wewe utauza bidhaa au la, faida wanapata kwa wewe kulipa laki saba na nusu then ukishindwa kuuza tafuta wengine walete lakisaba na nusu ili kupitia wao upate gawiwo,,,,,,,,mnabaki kuletana tuuuu
Nature ya hii biashara sio uuze sana bidhaa kupata faida, nature ya hii biashara ni kuingiza watu wengi kwenye chaneli yako ili upate faida, ukimuona mtu anang'ang'ana kuuza sana ujue bado mgeni au hajaiweka chaneli yake vizuri
Mtu aliejiunga toka inaanza maana yake hata wewe leo ukijiunga kwenye chaneli yake ukitoa tu laki saba maana yake anagawio lake hapo, na ndio maana atakwambia naingiziwa milioni tatu kwa mwezi, sasa mziki utakuja kubuma pale ma senior watakapokuwa wengi kuliko ma junior
Kifupi ni laki saba na nusu ndio inatakiwa ukifanikiwa kuuza manshalaaah, tusikae hapa tunadanganyana eti bidhaa za FL zitakutoa kimaisha kwa faida ya mauzo, kwamba ununue laki saba na nanusu uuze milioni kadhaa,,,,,,,,aah wapi
Kitakachokutoa ni kuingiza watu wengi kwenye chaneli yako.......not a damn products