Asilimia kubwa ya watu wamefanikiwa kupitia biashara, ni asilimia chache sana wana mafanikio kupitia ajira lakini wengi wenye majumba mazuri, magari na mali nyingine wamezipata kupitia biashara.
Siku zote elewa kwamba hakuna mfanyabiashara ambae atataka akwambie mafanikio yake na hata faida anayoipata katika biashara yake au aina ya wateja wake, wengi huwa na maneno ya kuonesha ugumu waliopitia lakini hawaoneshi njia aliyopitia hadi kupata mafanikio yake kibiashara na mara nyingi ukiwauliza kuhusu biashara husika hukimbilia kusema hailipi.
Kwa yule unaeanza usitegemee kwamba utaenda kumuuliza mfanyabiashara mbinu akakwambia za ukweli zaidi atakupa mbinu ngumu na changamoto kubwa ili umuone jinsi alivyo mpambanaji.
Hivyo basi unapotaka kuanzisha vibiashara inakubidi utenge muda na fedha za kutosha kufanya utafiti, tafiti kuhusu masoko ya bidhaa zako na nini hasa cha kuboresha katika bidhaa zako. Vile vile tafiti kuhusu sehemu ya kununua bidhaa, upatikanaji wake na urahisi wa usafiri.
Baada ya hapo anza kutafuta wateja wa kuuzia mzigo wako na mara nyingi hapa inakubidi ujenge kwanza uaminifu na jina ili uweze kushindana na wakongwe na mara nyingi unapoanza biashara yako hutakiwi kutengeneza faida kubwa bali wateja wengi, mfano kipindi wengine wanapata faida 10,000/= wewe unaweza kutengeneza faida ya 7,500/=kwa kushusha bei tofauti na wale uliowakuta , baada ya hapo unaweza kuanza biashara yako.
Siku zote usitegemee mawazo ya wanaofanya biashara husika pasipo kufanya utafiti wako mwenyewe, wengine hushauri ndivyo sivyo hali ambayo hupelekea kupata hasara.