Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
UKWELI HUWA HAUNA RAFIKI, SEMA UKWELI UCHUKIWE.
Lala pema peponi JEMEDARI NA RAIS WETU KIPENZI DKT JPM. wengine tushakataa kutubu wala kuomba msamaha kwa maana tunatambua kuzaliwa kwetu kuna makusudi na makusudi hayo haikuwa bahati mbaya.
Tulizaliwa mara moja na tutakufa mara moja bila kujali maumivu tutakayoyapitia ila hitimisho lake litakuwa ni umauti pekee.
Watanzania tulikupenda na kukuthamini; tungeambiwa kuwa unaumwa tungekuombea kwa imani zetu zote. Ila tuliambiwa ni mzima na tukaamini; maneno ya kuambiwa.
Sikuwahi kufikiria wala kuwaza na wala sikukubaliana na taarifa iliyotolewa kuwa umefariki. Nilihudhuria siku ya kukuaga; hakika niliamini kuwa ni wewe mwenyewe uliyelala kwenye sanduku lenye kioo.
Muonekano wako siku hiyo sintousahau maishani mwangu kamwe. Muonekano wako siku hiyo ulinifanya nitafakari namna nafsi yako ilivyokuwa ikiomba walau dakika kadhaa japo useme na Watanzania uliowapenda, naamini ulitaka walau uwaage; uwape kwaheri ya kuonana tena katika ulimwengu mwingine.
Nililikumbuka tabasamu na cheko lako pale unaposimama kuzindua mradi wenye manufaa kwa wananchi wako; hukuacha kututania. Nakukumbuka JOHN; nakukumbuka RAFIKI YANGU.
Rafiki yangu JOHN ulikuwa mtu wa kipekee sana. Uliweka utani mahali ambako panahitaji UTUO; hakika hotuba zako zilisikilizwa na wengi, tusiokuwa na TV tulienda kwenye vibanda umiza na kulipa kiingilio kukusikiliza na kukuona ukitumbua, ukirekebisha na kuonya. Ulikuwa kivutio na mtu wa kutolewa mfano mwema.
Ghafla taa ikazima; tukaingia GIZANI, sintofahamu ikatuingia, tukaambiwa umetutoka JOHN, ilikuwa GANZI kwa kila Mtanzania. Kama ilivyo kwa wengi na kwangu pia ilikuwa hivyo, sikuamini kuwa umetutoka JOHN.
Labda unipe MUDA DR. JOHN niweze kuandika kitabu chako. Nikuelezee kwa hisia zangu, namna nilivyokufahamu na namna ulivyozima ghafla. Niliwahi kushauriwa kupenda mtu kwa kiasi lakini kwako nilizama kabisa. Nilikupenda kupitiliza na nilikuamini kupitiliza na ndo maana nimeshindwa kukuondoa kwenye fikra zangu.
Kumbukumbu zako kwangu zipo nyingi, nimehudhuria matukio yako mengi ya kikazi.
Jioni ya leo nimekuandalia DUA maalumu kwa ajili yako. Nitakuombea RAIS WETU KIPENZI CHETU WATANZANIA WAZALENDO DKT JOHN JOSEPH MAGUFULI.