Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Wanasema msanii ni kioo cha jamii na kama unavyojua kioo hakibuni na kutengeneza taswira kutoka kusikojulikana bali huonesha taswira ya kitu kilekile kilicho mbele yake. Kwa lugha nyepesi ni kwamba kama msanii ni kioo cha jamii basi watuoneshayo kwenye muvi zao ni yale yale yaliyopo kwenye jamii husika. Natambua uwepo wa mambo ya kubuni na kufikirika katika muvi hizo lakini leo tuyaache hayo...
Nitajikita kwenye yale ambayo yanaweza kuwa kweli tu. Mimi ni mpenzi mtazamaji wa action movies sasa nimekuwa nikiona mambo haya yakijirudia rudia takriban muvi zote za ngumi nikaona si vibaya nikashare humu ili nipate ufafanuzi kama ni kweli yapo katika jamii au laa
1. Mtu anapata nafasi ya kummaliza kabisa yule anayeshambuliana naye lakini unakuta anampa nafasi ya kujaribu bahati yake kabla hajammaliza. 'Stelingi' na jambazi kuu ndio wanaoongoza hii tabia matokeo yake unakuta jitu linadhibitiwa lenyewe. Ngumi kavu kavu za mtu mbili ndio zinaongoza kwa jambo hili unakuta kaenda chini anasubiriwa aamke, au kamvizia vizuri badala ampe moja bila anaremba tena! Ni kweli wataalamu wa ngumi mna utaratibu huu au ni muvi tu?
2. Kufungua lock za pingu au kufuli kwa waya na/au pini. Movies nyingi tunaona watu wenye mafunzo maalumu ya kijeshi wakifungua makufuli na chains za polisi tena kwa njia ya haraka isiyokuwa ya kawaida. Hebu wataalamu tuambieni hili jambo lina ukweli wowote? Nikikumbuka zamani kufuli ya shaba ya "madeni china" ilivyokuwa inatutoa mafua pindi funguo inapopotea mpaka tunaharibu vitasa, siyo poa kabisa
3. Kwenye mashambulizi au mapigano yule kiongozi anakuwa wa mwisho kabisa tena hapa inarudi kama namba moja hapo juu hapo yaani mfano mtu kaja kuwavamia anawapiga mangumi ya maana lakini unashangaa kiongozi wa hawa wanaopigwa katulia tu tena ana bunduki pengine. Wanamalizwa wengine wee kisha ndo anatoa bunduki yake na pengine asiitumie hata akaleta mbwembwe nilizozisema kwenye namba moja. Hoja hapa nataka kujua je ni kweli nyinyi watu wa vita mkiwa eneo husika kwenye kushambulia mnadili kwanza na wadogo kisha ndo mje na wakubwa? Tena unakuta huyo mkubwa nae yupo hapohapo ground! Historia nyingi za vita tunapata kuona kinyume na hivyo kwani mara kadhaa zinaonesha wakuu wa adui wamekuwa wakishambuliwa mapema tu
4. Polisi kuliza ving'ora mfululizo wanapoenda au wanapokuwa eneo lenye uhalifu. Hii nayo naiona sana na huenda labda ni huku kijijini nilipo kunanifanya nione swala hili geni, watu wa Daslamu hebu nijibuni huko mjini hili jambo mnaliona? Baadhi ya muvi wahalifu au wale wazee wa kazi zisizohitaji kuonwa na raia wanafanya yao na wakisikia tu ving'ora wanakimbia polisi wanaambulia patupu
5. Askari wa usalama kutokupenda pesa ni jambo ninaloliona sana pia. Muvi nyingi unakuta mfano 'stelingi' katengeza pesa ya kutosha lakini mwisho wa siku majukumu yake yakikamilika anapotaka kuondoka anaigawa pesa yote kwa mtu aliyekuwa nae karibu eneo hilo katika kufanikisha mission. Kwamba hao watu wamekinahi mali kiasi hicho? Hii nashangaa maana askari wetu tunahadithiwa mara nyingi kwamba wanapora mali za watu wakiwa kwenye operations zao
6. Kuruka na parachute ni jambo ambalo nahitaji elimu ya kutosha sana ili nielewe. Unakuta mtu anaruka mzima mzima halafu hewani ndio anakadiria sasa akifika level ipi aachie parachute. Hiyo kidogo kwa mbali naweza kuelewa lakini ile ya kwamba kule hewani kabla ya kufungua parachute mtu anajigeuza atakavyo au anazungumza, wengine anajiset anakwenda kumkamata mwenzake asiye na parachute au analo akashindwa kulikontroo nk. Kwakweli matendo hayo huwa yananifikirisha kiasi maana huwa najaribu kujikumbusha nilivyokuwa mdogo na utundu wangu na serekasi zote lakini habari ya kutoka hewani kuja chini sijawahi kuona kama naweza kuicontol nikiwa angani
7. Kabla mtu hajauwawa anapewa "risala" ya kumuumiza au kumfungua ufahamu juu ya jambo fulani ambalo hakulijua kabla. Mfano jasusi amekamatwa unakuta au amewekwa 'telo' lakini hawamshuti wanaanza kumwambia nani kamsaliti mpaka akashikwa, njia watakayotumia kumuua na maneno mengine kibao ya kumuudhi. Wataalamu wa nyanja hizo hebu niambieni ni kwa nini inakuwa hivyo na je inakusudiwa nini kufanya vile maana ikiwa ni askari wanamfanyia mhalifu tunajua wanamtisha ili atoe ushirikiano lakini hii hakuna siri yoyote wanayohitaji
8. Mtu kupotezwa fahamu kwa sekunde 1 mpaka 3 ni jambo lingine ambalo silielewi. Unakuta mtu anawekwa kitambaa chenye dawa puani na mara tu kapoteza fahamu au anagongwa sehemu katika mwili mara moja tu tayari hana fahamu. Sambamba na hilo kuna lingine tena unakuta mtu anauwawa kwa dizaini hiyo hiyo kwamba hakukuruki wala hachukui muda ilihali mtu mwenyewe siyo mgonjwa mahututi wala nini tena unakuta ni komando kabisa. Madaktari na wataalamu wa ujasusi hebu niambieni hili jambo lina ukweli wowote?
9.