Ukweli kuhusu biashara

Ukweli kuhusu biashara

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Katika pitapita zangu nilikutana na watu waliojiajiri katika biashara zao tukawa tunabadilishana mawazo,mmoja akasema 'usiku wa manane ndio muda mzuri kwa wafanyabiashara/wenye makampuni kutathmini biashara zao kwa sababu kunakuwa na utulivu, pia mbinu mpya za kibiashara huwa zinakuja kichwani'.
Je,kuna ukweli wowote?
 
Ukilala ukiamka akili inakuwa fresh
Unauwezo wa kufanya stock kichwani bila vurugu za dunia
Bila miito ya simu,
Bila kelele za ndege
Bila sauti za magari
Wala bugdha yoyote.

Akili ikiwa na utulivu ni rahisi kupata mbinu mpya kwa kuwa unatafakari kitu kimoja kwa urefu na upana


Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli hata kama unataka uwasiliane na supplier nje ya nchi,ni muda muafaka.
 
Kunaweza kuwa na ukweli,kwa sababu nilishashuhudia jamaa mmoja alikuwa na kiwanda chake,yeye alikuwa anaenda ofisini saa nne usiku na ni umbali wa kama kilometre kumi na kitu hivi kutoka nyumbani kwake hadi ofisini.
 
Ha ha ha biashara gani ukiamka SAA 8 usiku unapata mbinu mpya labda mama
ntilie kesho uweke kitunguu
swaumu. But ukweli kuhus biashara ni kwamba.
Ukitaka watoto wako waishi vzr badae basi Fanya biashara , ni kitu ambacho wanaweza kuirithi ama kujifunza zaidi na wasijifunze kuwa watumishi wa umma ukubwani mwao.
Biashara ikifikia level fulani hivi,wewe unawatumia watu kukutajirisha kama kuwaajiri watu wenye taaluma zao,wewe unawapa dira tu kuwa unataka nini kifikiwe,na wanakuwa wanakupa ripoti ya utendaji wao.
 
Saa 11 jioni mpaka saa 5 usiku
Mimba mingi inatungwa huo muda
Mi binafsi kuanzia saa 5 usiku sijiruhusu nifanye jambo lolote zaid ya kulala labda iwe emergyency sana, hivyo najitaidi mambo yote nifanye chini ya mda huo matharani nawai kufungua biashara asubuhi sana na kuanza kazi kama kufunga hesabu na kuwasiliana na supplier, then usiku nikirudi hom huwa najitahidi niwe na note book yangu wakati nime relax na check tv. ndio huwa najitathmini na natathmini biashara kama kipo kitu cha msingi cha kuanza nacho au mtu wa kuwasiliana nae na note na kama kuna kitu sijakifanya sawa na note pia, issue ya stock ndani ya week huwa natenga siku moja kufanya hiyo kazi. To make long story short ni hayo...
Nb. Niko na shida moja nikichelewa kulala, mchana nakosa umakini katika biashara.
 
Mi binafsi kuanzia saa 5 usiku sijiruhusu nifanye jambo lolote said ya kulala labda iwe emergyency sana, hivyo najitaidi mambo yote nifanye chini ya mda huo maharani nawai kugundua biashara asubuhi sana na kuanza kazi kama kufunga hesabu na kuwasiliana na supplier, then usiku nikirudi hom huwa najitahidi niwe na note book yangu wakati nime relax na check tv. ndio huwa najitathmini na natathmini biashara kama kipo kitu cha msingi cha kuanza nacho au mtu wa kuwasiliana nae na note na kama kuna kitu sijakifanya sawa na note pia, issue ya stock ndani ya week huwa natenga siku moja kufanya hiyo kazi. To make long story short ni hayo....
Nakubaliana nawe,kila kitu ni mpangilio ila biashara inavyozidi kukuwa unajikuta yale majukumu uliyokuwa unayafanya wewe unaajiri watu.....kwa hiyo kwa upande wako unajikuta unatafuta muda wenye utulivu wa kukagua mahesabu,kuweka malengo mapya,pamoja na kufanya mawasiliano na ma-supplier wako kwa email/voice call ambao wako nje ya nchi.
 
Nakubaliana nawe,kila kitu ni mpangilio ila biashara inavyozidi kukuwa unajikuta yale majukumu uliyokuwa unayafanya wewe unaajiri watu.....kwa hiyo kwa upande wako unajikuta unatafuta muda wenye utulivu wa kukagua mahesabu,kuweka malengo mapya,pamoja na kufanya mawasiliano na ma-supplier wako kwa email/voice call ambao wako nje ya nchi.
Yaap, pengine utatafuta mda ambao hata wafanyakazi wako hawapo ili kuepuka movement na unnecessary disturbance ila mimi sijafika uko mkuu..
 
Yaap, pengine utatafuta mda ambao hata wafanyakazi wako hawapo ili kuepuka movement na unnecessary disturbance ila mimi sijafika uko mkuu..
Taratibu tutafika huko tu cha muhimu ni malengo na nidhamu katika matumizi.
 
Back
Top Bottom