Ukweli kuhusu bilioni nane za Jokate

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Wiki kadhaa zilizopita vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania, vilitawaliwa na habari ya mwanadada Jokate Mwegelo kuingia mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni Nane za kitanzania na kampuni ya kichina.

Baada ya habari hii kutoka magazeti mengi ya kibongo pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii imekuwa ikiripoti kuwa Jokate anamiliki kiasi hicho cha pesa.

Kuna kitu amacho sijakielewa vizuri bado.Ni kwamba Jokate amepewa Shilingi BILIONI NANE au ameingia mkataba wa kibiashara wenye thamani ya shilingi bilioni nane ? Hebu tuwekane sawa hapo wadau coz ninavyo jua mimi kuna tofauti kubwa sana kati ya "kupewa shilingi bilioni nane " na kuingia mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni nane..

Ninacho kiona hapo ni kwamba, Jokate hana wala hajapewa hizo shilingi bilioni nane kama inavyo ripotiwa kimakosa na baadhi ya vyombo vya habari nchini,isipokuwa ameingia mkataba wa biashara wenye thamani ya shilingi bilioni nane.

Kwa lugha nyingine ni kwamba,Jokate ameingia kwenye mkataba wa biashara na kampuni hiyo kuzalisha,na kusambaza bidhaa zake kwa kipindi fulani,eidha mwaka mmoja au miaka mitano. Endapo bidhaa hizo zitafanikiwa kuingia sokoni na kuuzwa,baadhi Jokate atapata gawio lake ambalo jumla yake itakuwa shilingi bilioni nane.

Hivyo ndivyo nilivyo elewa mimi.Kwa mlio elewa tofauti hebu nifafanulieni hapo ili nipate kujifunza.
 
Mm pia nimeelewa hivyo mkuu, unless kama amepewa hizo hela ziwe mali yake bila shaka vyombo vya habari vingeripoti kuwa amesaidiwa mtaji wenye thamani hiyo.... hapa nafikiri yy anabaki kuwa ni supplier wa hizo bidhaa kwa hapa Tanzania.
 
Mm pia nimeelewa hivyo mkuu, unless kama amepewa hizo hela ziwe mali yake bila shaka vyombo vya habari vingeripoti kuwa amesaidiwa mtaji wenye thamani hiyo.... hapa nafikiri yy anabaki kuwa ni supplier wa hizo bidhaa kwa hapa Tanzania.

Yeah hapo tunaenda sawa mkuu.
 
hata mie nimeelewa hvyo kwa kweli ila hongera zake namkubali sana
 
Mm pia nimeelewa hivyo mkuu, unless kama amepewa hizo hela ziwe mali yake bila shaka vyombo vya habari vingeripoti kuwa amesaidiwa mtaji wenye thamani hiyo.... hapa nafikiri yy anabaki kuwa ni supplier wa hizo bidhaa kwa hapa Tanzania.

Noted mkuu.... asiye elewa ufafanuzi wako basi kichwa mlenda kama sio bichwa mbege.
 
hata sijui! yey ndio anaejua ukweli! hata hvyo siku akiwa anaingia nao mikataba sikuwepo
 
What if katika huo mkataba wanatakiwa wampe robo ya pesa ili aweze kufanya hiyo biashara?

mimi nafikiri inategemeana sana na aina ya mkataba.......
 
Hebu fafanua vizuri hapo kaka, alimaanisha nini?

Nas alikuwa anasema amejaza "paper" kwenye briefcase, ila usifikiri hela, maana hela zake briefcase halitoshi, kajaza bank statements.

Mwacheni mjasiriamali ajaribu, jungu kuu halikosi ukoko.

Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
 
Jokate bwana hivi yule bilionea wa darling alishampiga chini ?
 
Na mimi naomba kuuliza swali, hivi wanavyosema mchezaji kasainishwa mkataba wa milioni mia tano, je ndo anapewa zake au ni makaratasi tu?
 
Kilichotokea katika hili ni ameingia mkataba na mchina huyu kama mwekezaji ambapo ni uwekezaji wenye thamani ya 8bn. Katika uwekezaji huo kitajengwa kiwanda kitakachokuwa kinazalisha bidhaa zinazosambazwa na kampuni yake ya Kidoti.
 
Kilichotokea katika hili ni ameingia mkataba na mchina huyu kama mwekezaji ambapo ni uwekezaji wenye thamani ya 8bn. Katika uwekezaji huo kitajengwa kiwanda kitakachokuwa kinazalisha bidhaa zinazosambazwa na kampuni yake ya Kidoti.

Hilo ndio jibu,Jokate hizo bilioni nane atazisikia kwenye bomba tena la gesi mtwara au la maji bagamoyo,atachopata ni wazungu wanaita dividend tu(Gawio la faida kulingana na makubaliano waliyofikia).
 
Full of paper, not money it's bank statements... - Nas

Heri ya mwaka 2015 kaka! Ni kama amepewa fursa ya kuonyesha uwezo wake wa namna ya kucheza na vitu/biashara yenye thamani ya hizo pesa zilizoainishwa kwenye mkataba. Ana wajibu wa kutekeleza!
 
Ningeomba tufuatilie makala za Jokate.
Huyu Dada anajituma sana na sio masifa ya kijinga kama Mrs. Ngololo

Jokate Kichwa cha maana,niliwa kufuatilia mahojiano yake kadhaa ndio niligundua ana kitu kichwani.
Tutambue kwamba Samaki hatafutwi nchi kavu,akishafika nchi kavu ujue aliishatafutwa.Dada anahangika huyu.
Na angekuwa masifa basi alikuwa na nafasi ya kila siku kuwa magazetini,lakini inaonekana aijua kwamba pesa anazolipwa na wamiliki wa magazeti wauze habari zake hazina issue zaidi ya kumporomosha,na kuamua kujituma kwa nguvu zake na kuonyesha juhudi zake.

Huwezi kusaidi kama huna Idea nzuri na juhudi ya kumuonyesha mwenye mtaji kwamba wewe kama wewe umefanya nini ili na yeye awe impressed.

Dada Hongera sana nakumbuka mahojiano yako niliwahi kuona EATV,ninaona kwamba utafanikiwa kwa uwezo wa mungu maanauna dhamira za mbali sana.

Bongo maneno kawaida tu,wewe kusanya mpunga kula bata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…