LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 18,037
- 33,681
Wiki kadhaa zilizopita vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania, vilitawaliwa na habari ya mwanadada Jokate Mwegelo kuingia mkataba wenye thamani ya shilingi Bilioni Nane za kitanzania na kampuni ya kichina.
Baada ya habari hii kutoka magazeti mengi ya kibongo pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii imekuwa ikiripoti kuwa Jokate anamiliki kiasi hicho cha pesa.
Kuna kitu amacho sijakielewa vizuri bado.Ni kwamba Jokate amepewa Shilingi BILIONI NANE au ameingia mkataba wa kibiashara wenye thamani ya shilingi bilioni nane ? Hebu tuwekane sawa hapo wadau coz ninavyo jua mimi kuna tofauti kubwa sana kati ya "kupewa shilingi bilioni nane " na kuingia mkataba wenye thamani ya shilingi bilioni nane..
Ninacho kiona hapo ni kwamba, Jokate hana wala hajapewa hizo shilingi bilioni nane kama inavyo ripotiwa kimakosa na baadhi ya vyombo vya habari nchini,isipokuwa ameingia mkataba wa biashara wenye thamani ya shilingi bilioni nane.
Kwa lugha nyingine ni kwamba,Jokate ameingia kwenye mkataba wa biashara na kampuni hiyo kuzalisha,na kusambaza bidhaa zake kwa kipindi fulani,eidha mwaka mmoja au miaka mitano. Endapo bidhaa hizo zitafanikiwa kuingia sokoni na kuuzwa,baadhi Jokate atapata gawio lake ambalo jumla yake itakuwa shilingi bilioni nane.
Hivyo ndivyo nilivyo elewa mimi.Kwa mlio elewa tofauti hebu nifafanulieni hapo ili nipate kujifunza.