Ukweli kuhusu degree ya miss Tanzania

mwambojoke

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
1,084
Reaction score
647
Katika pita pita zangu mitandaoni nimekutana na hii Video ya Miss Tanzania. Kipindi ambapo anatafutwa miss kinondoni. Ni kweli alisema ana miaka 18 lakin hakusema kuwa ana degree. Zaid alichosema ni kuwa yeye ni Applicant wa IFM. Sasa sijajua hiz rumors zinatoka wapi. Please cheki hii video kuanzia dk ya 8.

Miss kinondoni 2016.


Ni kwa taarifa tu.
 
TAARIFA KWA UMMA

Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;

1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.

2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.

3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo.

4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya "Character assassination" lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.

Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atuletee Taji la Dunia.
Ni msichana Asiye na bwana wala boyfriend na hajui mwanaume i.e mwanamwali!
Kwa maelezo yake mambo hayo ataanza baada ya kumaliza masoma na kufanya kazi miaka minne!

Ahsanteni.

Charles William
Kaimu Ofisa Habari wake.
0716719589
 
Ahsante sana.
 
Tz kwa polojo hatari yaani hutupendi mambo mazuri ya mtz mwenzetu kila kitu kupinga tena roho mbayaaa tuu kuna mijitu kweli haikutakiwa kuishi na kuzaliwa hapa nchini jamani wanamchafua mtoto wa watu bure. Kila kitu siasa ya siasa tz ni majanga. Pole Dada we songa mbele.
 
Hapo uliposema hana mwanaume wala boyfriend halafu ukaongozea kuwa diana ni mwanamwali dah......Mimi hapo naona umetudanganya coz kumpata mwanamwali katika miss tanzania sidhani kama ilisha/itakuja kutokea anyway siri hiyo aijuaye ni Mungu tu na yule atakayekuja kumwonja.
 
Hapo mwisho tu, labda asiwe na ushoga na kina wema na wenzake, atakuja kuwa zaidi yao japo simuombei mabaya, upuuzi kuwa baada ya mwaka Ile rangi yake haitakuwepo tena
 
Hapo ya uana wali unamtafutia shida mtoto wa watu, hapa mapapa, manyangumi fataki yatamsumbua sana
 
Ndo zari lake hlo maneno mingi ndo kapenya ivo miss tz
 
ofisa habari kanjanja wewe,unatuletea porojo zilezile,weka evidence mfano vyeti chake tuone
 
Was is it necessery kuutangazia uma kama binti ni mwanamwali?

Majaji wanajihami tu. Twajua ili kufikia hata jina lako kuitwa kuingia kwenye bas lao tiyari ushatobolewa na majaji ka 7 hivi. Vyumba vya mahoteli vina siri kuubwa. Usiende kujidhalilisha
 
Sasa wewe mtoa taarifa wanaume wake wanatuhusu nini mpaka umwanike hapa jukwaani kwa aibu kiasi hiki!!!

Akianza kubembwa na wakubwa mlalamike kuwa hajatulia wakati hapa inaonesha mnampigia promo apate wanaume.

Dah, kweli tz ni zaidi ya unavyoijua.
 
Umefafanua vizuri, ila hapo kwenye red, naona umevuka mpaka, huu uafisa habari ni wa mwendokasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…