Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi πŸ’”

Rubish .kama kiwanja kilikuwa cha mwanamke kulikuwa na haja gani ya kubadilisha hati.kwa nini huyo mwanamke alikubali nyumba ijengwe kwenye kiwanja hicho?
Kwa nini hakumwambia atafute uwanja mwingine ndo ajenge.huoni huyo mama hakuwa na nia nzuri kubadilisha hati ya uwanja.kwani hati ingekuwa yao wenyewe watoto hawangeirithi.
 
Kuna tofauti kati ya kuhamisha umiliki wa majengo na viwanja kwa watoto na kushirikisha watoto kwenye biashara zako.
Angalia tofauti ya kile ulichoandika kwenye post yako ya awali hiki ulichoandika sasa.

Alichofanya Jane ambacho wewe umeridhia ni kuhamisha umiliki wa jengo na sia biashara zake.
Hicho ndicho hasa tunacho shindania.

Hata hiyo biashara huwezi kumkabidhi au kumshirikisha mwanafunzi wa miaka 16 kama walivyo watoto wa Kweka na Jane.

Ni kweli tunatakiwa hasa tuwashirikishe watoto wetu kwenye biashara zetu.
Lakini kuna tofauti kumilikisha majengo na kushirikisha watoto kwenye biashara.

Hata huyo Mzee Ghulam Dewji ameshirikisha watoto wake kwenye shughuli zake baada ya watoto hao kumaliza masomo yao.
 
huu uzi ni wa upande wa k , je upande wa me vipi, hapa kwa vyovyote vile mwanamke alitaka kumzidi speed me,
 
Mimi huwezi kunifananisha na huyo mpuuzi...
Nimetoa mfano , endapo huyo dada angekuwa ndugu yangu kwa namna yeyote ningemmaliza huyo jamaa... maana ana deserve...

Changamoto anazopitia isiwe chanzo cha kuua mtu, tena mkewe ambae wamezaa watoto?

Hata nikiwa katika nafasi ya Kweka siwezi kuua mtu kisa ugomvi wa nyumba... kufanya kisasi haimaanishi sina uwezo wa ku control emotions zangu...

Kweka anyongwe, asiponyongwa ndugu za Jane wamalizane nae...
 
Ukimsikiliza dada yake Jane wa tumbo Moja kaongea kwa busara sana lawama zimedondokea kwa Jane kumbe kesi sio ya leo ni ya muda na alishauriwa na alikua kinacho enda kitokea
Katika familia ya Urassa huyu dada yake Jane peke yake ndio anaonekana ana hofu ya MUNGU , pasipokujali aliyeuwawa ni mdogo wake wa damu lakini kaamua aweke wazi ukweli wa mambo ulivyo...
 
Katika familia ya Urassa huyu dada yake Jane peke yake ndio anaonekana ana hofu ya MUNGU , pasipokujali aliyeuwawa ni mdogo wake wa damu lakini kaamua aweke wazi ukweli wa mambo ulivyo...
Kuna kingine kimejificha zaidi ya umiliki wa hiyo nyumba. Naamini ni uchepukaji na kiburi!
 
Hati ya nyumba tayari ilishatoka mkuu ikiwa na majina ya watoto - hata mke hakua mmiliki bali msimamizi tu mpaka mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18.
Kama ni hivyo, kwamba lengo la Mke ni Nyumba hiyo kumilikiwa na Watoto na sio yeye Wala mume...... mbona Mke hakutumia busara ya kuΓ ndika Majina ya Mume na Mke kama wasimamizi, na Watoto kama Wamiriki mpaka watapofikisha miaka 18...?
 
Jane Urassa alikuwa mjinga, lakini Laurent Kweka naye kaamua kuhitimu ujinga kwa vitendo! πŸ˜‚πŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈ

Yaani badala ya kutatua matatizo kwa akili, risasi ndiyo imekuwa suluhisho?

Hii siyo hasira tena, ni akili kuchukua likizo ya kudumu! πŸ˜…


Ukatili hauna utani, na hakuna ugomvi unaostahili kuishia kwa mauaji.
 
Sasa Hapo ungekuwa na tofauti gani na Kweka?
Unasema Kweka ana deserve kuuliwa kwakuwa kaua na wewe ukiua uta deserve kuuliwa
Hapo itakuwa wote mmeshindwa Ku handle changamoto katika namna yakutokuongeza changamoto zingine
 
Ila nyie wanawake ni wabinafsi sana aisee
 
Hakuna anayependa kuua bwana labda wanajeshi vitani na polisi wakiwa kwenye mission za majambazi yenye siraha.

Kama waliishi miaka 18 iweje auliwe wakati huu?

Kuna jambo lilipelekea kitendo hicho kufanyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…