Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi πŸ’”

Nimeshasikia mengi sana kuhusiana na mkasa huu, ila ki ukwel inaonekana marehem alikuwa mbinafsi sana, hakutaka nyumba iwe ya familia (baba, mama na watoto) ila alitaka iwe yake yeye na watoto pekee!

Inakuwaje mpo katka ndoa halaf baba ambae ni kichwa cha familia anatengwa katka umiliki, et kisa mwanamke ndo kanunua kiwanja na kujenga, mbona sis wanaume unapokua na mali zinahesabika ni mali za familia (na mke akiwemo)!?

Ila kuna wanaume wananyanyasika sana katka ndoa zao, sema machoz na maumiv yao hakuna anayeyajali!
 
Exactly, wakati huo mpo uchi ,machine imebanwa KWENYE mapaja , hata namba ya Siri unaisahau ghafra mwanamke ndo anakukumbusha
 
SWALI (hasa kwa wanaume walioreply wakiunga mkono mauaji na huyu mama kwenye nyuzi zilizopita)
  • JANE ALIKOSEA NINI?
  • NI NINI KIFANYIKE ILI MAUAJI NA UKATILI KAMA HUU USIENDELEE KUTOKEA?
Usichokijua Bunju hakuna kiwanja cha milioni hamsini lakini kuna viwanja vyenye nyumba za million 350 sasa upige hesabu kichwani Jane anunue kiwanja Tsh 1,700,000/= Kweka ajenge nyumba ya Tsh 350 mill mwisho Jane abadili jina lisisomeke Kweka family lisomeke Jane&Familly.

Hata kama mimi wewe sikuachi kichwa chako mali yangu i swear!
 
Source ya habari sio ukweli wote.
Ni kweli hatuwezi kuujua ukweli wote, Laurence na Jane ndiyo wanajua.
Maswali,
1. Kama kiwanja lilikuwa cha mwanamke na nyumba alijenga mwanaume nini kilisababisha mwanamke atengeneze hati yenye jina lake na watoto tu akimuacha mwanaume nje ??
Jane si mmiliki bali msimamizi mpaka mtoto wao wa kwanza (15 years old) atakapofikisha miaka 18.
Wote yeye na mumewe hawakuwa wamiliki, na Lawrence ndiyo alikua anapinga hilo.
 
Jane kanunua kiwanja kabla ya ndoa na ameolewa 2008 ni kitambo kidogo so naelewa unachosema kuhusu thamani.

Ila sheria za umiliki zinasemaje? nani ni mmiliki, mwenye kiwanja au aliyejenga?

Enewei, Jane hakuandika jina lake kwenye hati, hata yeye si mmiliki bali msimamizi tu mpaka watoto watakapofikisha miaka 18 (usimamizi wake ulikua unaisha baada ya miaka 3, mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18).

Ila nafikiri ile kasumba ya watoto ni wa mama, hata kama hati ikiwa kwenye jina la watoto bado mama atanufaika zaidi ndiyo ilimfanya Kweka asikubaliane na swala la kuandika majina ya watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…