Ukweli kuhusu kesho ya taifa la Tanzania

Ukweli kuhusu kesho ya taifa la Tanzania

Edgar Kyando 34

New Member
Joined
Jun 3, 2024
Posts
4
Reaction score
1
Tanzania ni nchi iliyo na amani upendo na mshikamano baina ya jamii na serikali Kwa ujumla.katika miongo tofauti imekua iki ongozwa na viongozi tofauti na wote wamechangia ukuaji wa nchi katika nyanja tofauti ,uchumi ,siasa kilimo ,uvuvi na katika biashara . Ningependa kuelezea changamoto ambazo huwenda ziki tatuliwa vyema ita saidia katika ujenzi wa Taifa la Tanzania ( Tanzania ya Uchumi wakati )

1. Kuto wajibika Kwa Viongozi , viongozi wengi katika nchi ya Tanzania hawana moyo katika kuwajibika kutimiza majukumu yao katika sehemu wanazo pangiwa hivyo Ina lazimu viongozi wengine kuanzisha kampeni za kusahihisha na kufichua maovu yanayo fanywa na watu wengine , mfano oparesheni inayo ongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul makonda Ina changia kuongezeka Kwa gharama katika serikali na upotevu wa muda hii yote ni sababu viongozi wanao teuliwa sio wawajibikaji katika kutekeleza majukumu yao. Hivyo basi ni muhimu serikali kuangalia namna Bora ya kuchagua viongozi wenye sifa na wanao weza kuwajibika ipasivyo .

2. Sheria katika uchaguzi wa viongozi , Tanzania ni nchi ambayo imesha piga hatua kidogo katika siasa , napendekeza serikali iangalie namna Bora kutumika katika kuchagua viongozi wake , mfano Sheria katika ugombezi wa Ubunge , mbunge ana ruhusiwa kugombea akiwa na elimu ya darasa la saba kwamba ana jua kisoma na kuandika , hivyo tuna shindwa kutatua matatizo ya wananchi Kwa ufasaha kwani ulimwengu wasasa unahitaji kutumia watu wenye elimu zaidi kuweza kuliongoza taifa mfano , Mbunge wa Mara alionekana aki kosoa uwepo wa Fedha ya kujikimu katika vyuo ,hii huenda ni kwasababu hakuwahi kufika chuo na kuangalia namna fedha inatumika katila kuendesha elimu ya vijana nchini , pia wabunge wengi wakiwa wanafanya shughuli za kutatua changamoto hawana uta tuzi mzuri katika kutatua changoto zinazo zikumba jamii , mfano mzuri upo utofauti wa maendeleo katika majimbo baina ya wabunge walio na elimu na wabunge wasio na Elimu . Hivyo napendekeza uboreshwaji wa Sheria mpya katika ugombezi wa Ubunge na udiwani ili ilete tija katika maendeleo ya Taifa la Tanzania.

3. Rushwa , Hili ni Tatizo kubwa katika taifa la Tanzania kwani limeanzia chini ( ngazi ya kata ) Ofisi nyingi za Tanzania ili uweze kupata Huduma Kwa haraka Ina kugharimu utoe chochote ndio uhudumiwe Kwa haraka , hivyo ina sababisha ,kudorola Kwa uchumi wa Taifa kwani hupelekea utoaji wa Huduma mbovu Kwa jamii , matumizi mabovu ya rasilimali za Taifa , napendekeza namna ya kutatua tatizo Hili ikiwa limekua ni tatizo sugu Kwa miaka mingi , ( i . Iundwe Sheria kwa atakaye jihusisha na rushwa afungwe zaidi ya miaka 30 (TAKUKURU) , au ahukumiwe kifo . ii Uwekwaji wa Namba za simu pia zinazo patikana katika office zinazotoa Huduma kwajamii)
Screenshot_20240604-143324.png


4. Katiba ya nchi ya Tanzania , katiba inayo tumika katika taifa la Tanzania ni ya kutoka mwaka 1972 , hii nikatiba iliyo undwa na wazee wa miaka ya zamani ,na ulimwengu wa sasa nitofauti na zamani hivyo basi Katiba ya mwaka 1972 haiwezi kuwa na tija kuongoza jamii ya watu wa 2024. Serikali inaweza kuangalia namna Bora ya kuweza kubadili katiba ya nchi kama Inavyo pendekezwa kuwa katika pendekezo ikipitishwa inaweza kuwa na Tija katima maendeleo ya Taifa hili.

5. Uwepo wa vyama vya kuwezesha vijana wa jinsia ya kiume na kike , nchi ya Tanzania imekua ikitumia jitihada kubwa katika kuhakikisha Wana wawezesha watoto wakike katika nyanja tofauti na kuwa acha mbali watoto wa kiume hivyo taifa haliwezi kujingwa na Wanawake tuuu , Kwa kuangalia baadhi ya vikundi vingi vilivyopo nchini ni vikundi maalumu Kwa ajiri ya wanawake mfano TAMWA , TAWLA ,WAT , hivyo basi serikali iangalie namna Bora katika uwezeshaji wa vijana Kwa kuangalia usawa wa kijinsia .

6. Tatizo la Ajira nchini , Kwa Sasa ina sadikika ili kijana aweze kuajiliwa katika sekta yeyote nchini inabidi awe na mtu wa kumuunganisha (connection). Hivyo inapelekea uwepo wa watendaji kazi ambao hawana vigezo vya kua wafanyakazi katika ta asisi , vijana wengi wenye uwezo mzuri na vigezo sitahikinhuishia kuwa mtaani , na wasio na uwezo kuwa maofosin hivyo basi tunakua na viongozi au watendaji wanao shindwa kutimiza majukumu mwishowe Huduma mbovu Kwa jamii na pia kukatisha moyo vijana wanao wenye uwezo na vigezo katila kulitumiakia Taifa.

7. Namna Bora katika Kuta tua matatizo ya wananchi , namna inayotumika hivi karibuni na viongozi wengi ni namna ambayo IPO kama kampeni za kisiasa kwani viongozi wengi wamekua waki tumia majukwaa na kuanzisha kampeni za kutatua changamoto kwa kuwa kusanya watu na kuanza kufichua maovu yanayo fanywa na viongozi , hii inaleta taswira kuwa serikali ipo kufanya kampeni za mwaka wa 2025 , hivyo basi namna Bora ya kutatua matatizo ya wanachi ni kama wanachi Wana hitaji jambo Fulani wapew kama ni mbolea ,pembejeo , n.k , viongozi waki kosea waondoshwe katika cheo alicho nancho na kuhukumiwa mara moja .ita tusaidia kujenga taifa Bora litakalo weza kufika katika uchumi WA kati.

8. Matumizi ya Rasilimali zilizopo nchini katika kuijenga nchi kuliko kutumia Fedha za kukopa kutoka mataifa ya ughaibuni , Nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwa na Rasilimili nyingi ila Kuna tatizo katika namna ya utilization of resources , takwimu Zina onyesha Deni la taifa ni zaidi ta tirion 72 , hivyo Kuna uwezekano ika tuletea matatizo katika nyanja tofauti ikiwemo uchumi na jamii mfano kulazimishwa kutumia utamaduni wa ughaibuni ambao ni haramu katika utamaduni wetu ( Ushoga) . Serikali iache kukopa pesa na kuamua kutumia rasilimali vizuri katika kutoa huduma kwa jamii.

9. Vyama vya siasa kutumia nguvu kuliko hoja , Tanzania ni taifa linalotumia mfumo wa vyama vingi katika siasa katika kuliendesha taifa hivyo baadhi ya vyama hutumia nguvu pale wanapo zidiwa hoja na vyama vingine hatimae hupelekea watu kupotea mfano Beni saa nane alikua ni mwana harakati upande wa chadema ambaye alipotea na haeleweki Yuko wapi Hadi Leo , Baadhi ya wafuasi wa vyama wamekua waki kamatwa na kuwekwa polisi akiwemo Mdude , mwabukusi .serikali inahitajika kuangalia namna Bora ya kuweka uhusiaono ulio Bora kwa ajiri ya kujenga taifa lenye kufikia uchumi wa kati , kwani vyama vyote lengo la ninkujenga nchi .

10. Uboreshwaji wa Sheria na mazingira katika sekta ya biashara , matumizi ya risiti za EFD zimekua kuwa ni kikwazo kikubwa kwa wafanya biashara wa Tanzania hivyo imepelekea baadhi ya wafanya biashara kukimbilia nchi Jirani ilinkuweza kufanya biashara mfano mkoa wa songwr mji wa Tunduma wafanya biashara wengi wame kimbilia nchini Zambia ili waweze kujikwamua kibiashara kutokana na kua na mitaji midogo huku utoaji wa risiti za EFD kuwalazimu walipie ushuru mkubwa zaidi hata ya mitajii yao .hivyo basi ni vyema serikali kuangalia namna Bora ya kutatua changamoto kama hizi na kuweka mazingira mazuri kuwavutia wafanya biashara kufanya biashara nchini

11. Utekelezwaji wa Taarifa inayo tolewa na CAG bungeni .
CAG hutoa taarifa bungeni ambayo huusisha taasisi tofauti za kiserikali na zisizo za kiserikali. Mfano taarifa ya CAG 2023 ili bainisha baadhi ya taasisi kuwepo na ubadhilifi WA Mali za umma lakini bado wahusika awajachukuliwa hatua ,ningependa kushauri serikali ya Tanzania ichukue hatua kwa wote wanao husika ili tuweze kuijenga Tanzania yenye manufaa siku zijazo .

Mwisho , kama Taifa la Tanzania lita fanikiwa kutatua changamoto hizo Kuna uwezekano mkubwa wa kujenga Taifa lili Bora miaka ijayo.

( Mungu bariki Tanzania )
 
Back
Top Bottom