Samahani wadau ambao ni manguli wa historia, naomba mnipe ukweli kuhusu mwisho wa vita ya pili ya dunia na kifo cha adolph hitra na alizikwa wapi???
Nisaidieni hili
Adolf Hitler The Fuhrer!
Alifikia hatma ya Kujiua kama inavyoelezwa na vyanzo vingi vya habari mnamo mwaka 1945 akiwa pamoja na Mkewe Eva Braun,
Hata hivyo habari hizi za Hitler kujiua zinamashaka makubwa sana kwa sababu Masalia ya Mwili wake wala ya mke wake hayajawahi kupatikana kabisa.
Wazee wa Nadharia ya Njama wanadai kuwa Hitler alifanikiwa kutorokea Amerika ya Kusini kama jinsi baadhi ya Maofisa wake SS walivyofanya kwa mfano
Adolf Eichmann ambaye baadae alitiwa mikononi mwa Mossad wakati wa operesheni finale ya akina
Rafael Eitan.na kupelekwa Israel kukabili mashtaka ya Uhalifu wa Kivita.
Professor Hugh Trevor Roper wa Chuo Kikuu cha Oxford ni kati ya wana historia waliopata nafasi kwenda Ujerumani kufanya Utafiti wa hatma ya Hitler baada ya vita vya Pili vya Dunia.
Alikuja na Kitabu
"The Last Days of Hitler"
Hugh Trevor Roper anadai katika kitabu chake kuwa Hitler alijiua kwa Kujipiga Risasi na Mkewe Eva Braun alijiua kwa Kunywa Sumu aina Cyanide.Na alitoa maelekezo kuwa miili yao ichomwe moto kwa Maafisa wake.
Habari zingine zinadai kuwa General
Georgy Zhukov Kamanda wa Majeshi ya Urusi {Red Army}.Kumbuka kuwa Jeshi la Urusi ndio lililokuwa la kwanza kuingia Berlin na Kuanza kamata kamata ya wafungwa wa kivita wa jeshi la Manazi Jamaa aliruhusu uwazi sana juu ya wale wote waliotaka kujua kuhusu Hitler na hii haikumfurahisha Bosi wake Joseph Stalin hivyo aliitwa mara moja arudi Moscow kupangiwa kazi ingine na akaletwa Kamanda mwingine akiwa na maelekezo ya kuchanganya kabisa habari zozote zilizomhusu Hitler.
Stalin alihofia sana kuwa iwapo watatangaza kuwa Hitler amekufa,mtu ambaye alikuwa adui pekee aliyewaunganisha Mabepali na Wakomunisti kupigana bega kwa bega italeta shida kwa upande wa USSR kuanza kupambana na Mapebali mapema sana.
Hivyo "Uzushi" wa kuwa Hitler bado yuko hai umeendelea kuwepo na kufurahiwa sana na Warusi.Wakidai kuwa Iwapo Mabepali wangeamini kuwa Hitler ni mzima wangekosa Ujasiri na kuendelea kuamini kuwa Adui yao yupo hai anajipanga kwa Uovu wowote ule.
Hivyo Ndio maana hear says ni Nyingi sana kuwa Hitler alitorokea Amerika ya Kusini na aliishi mpaka kuja kufa kifo cha Uzee.
Iwapo Hitler angelikuwa Hai - Lazima Mossad wangemkamta kama jinsi walivyowakamata SS officers wengine kote duniani.
Nadhani nimejaribu.