Ukweli kuhusu kifo cha Adolf Hitler

Ukweli kuhusu kifo cha Adolf Hitler

Walimfanyia surgery kumbadilisha sura kuwa mtu mweusi,inasadikika yupo Huku Africa.
 
Kuna story zingine zinasema Adolf Hitler alifanikiwa kutoroka na shehena kubwa ya dhahabu yuko hai Brazil mafichoni
ef28e27f3c1d5e566cf8b8679d5385dd.jpg
Ni Argentina sio Brazil
 
kuna Hitra
kuna Hitle
hii dunia ilijaa wauaji
 
Samahani wadau ambao ni manguli wa historia, naomba mnipe ukweli kuhusu mwisho wa vita ya pili ya dunia na kifo cha adolph hitra na alizikwa wapi???
Nisaidieni hili

Adolf Hitler The Fuhrer!
Alifikia hatma ya Kujiua kama inavyoelezwa na vyanzo vingi vya habari mnamo mwaka 1945 akiwa pamoja na Mkewe Eva Braun,
Hata hivyo habari hizi za Hitler kujiua zinamashaka makubwa sana kwa sababu Masalia ya Mwili wake wala ya mke wake hayajawahi kupatikana kabisa.

Wazee wa Nadharia ya Njama wanadai kuwa Hitler alifanikiwa kutorokea Amerika ya Kusini kama jinsi baadhi ya Maofisa wake SS walivyofanya kwa mfano Adolf Eichmann ambaye baadae alitiwa mikononi mwa Mossad wakati wa operesheni finale ya akina Rafael Eitan.na kupelekwa Israel kukabili mashtaka ya Uhalifu wa Kivita.

Professor Hugh Trevor Roper wa Chuo Kikuu cha Oxford ni kati ya wana historia waliopata nafasi kwenda Ujerumani kufanya Utafiti wa hatma ya Hitler baada ya vita vya Pili vya Dunia.
Alikuja na Kitabu "The Last Days of Hitler"

Hugh Trevor Roper anadai katika kitabu chake kuwa Hitler alijiua kwa Kujipiga Risasi na Mkewe Eva Braun alijiua kwa Kunywa Sumu aina Cyanide.Na alitoa maelekezo kuwa miili yao ichomwe moto kwa Maafisa wake.

Habari zingine zinadai kuwa General Georgy Zhukov Kamanda wa Majeshi ya Urusi {Red Army}.Kumbuka kuwa Jeshi la Urusi ndio lililokuwa la kwanza kuingia Berlin na Kuanza kamata kamata ya wafungwa wa kivita wa jeshi la Manazi Jamaa aliruhusu uwazi sana juu ya wale wote waliotaka kujua kuhusu Hitler na hii haikumfurahisha Bosi wake Joseph Stalin hivyo aliitwa mara moja arudi Moscow kupangiwa kazi ingine na akaletwa Kamanda mwingine akiwa na maelekezo ya kuchanganya kabisa habari zozote zilizomhusu Hitler.

Stalin alihofia sana kuwa iwapo watatangaza kuwa Hitler amekufa,mtu ambaye alikuwa adui pekee aliyewaunganisha Mabepali na Wakomunisti kupigana bega kwa bega italeta shida kwa upande wa USSR kuanza kupambana na Mapebali mapema sana.

Hivyo "Uzushi" wa kuwa Hitler bado yuko hai umeendelea kuwepo na kufurahiwa sana na Warusi.Wakidai kuwa Iwapo Mabepali wangeamini kuwa Hitler ni mzima wangekosa Ujasiri na kuendelea kuamini kuwa Adui yao yupo hai anajipanga kwa Uovu wowote ule.

Hivyo Ndio maana hear says ni Nyingi sana kuwa Hitler alitorokea Amerika ya Kusini na aliishi mpaka kuja kufa kifo cha Uzee.

Iwapo Hitler angelikuwa Hai - Lazima Mossad wangemkamta kama jinsi walivyowakamata SS officers wengine kote duniani.
Nadhani nimejaribu.
hitler100.jpg
 
Samahani wadau ambao ni manguli wa historia, naomba mnipe ukweli kuhusu mwisho wa vita ya pili ya dunia na kifo cha adolph hitra na alizikwa wapi???
Nisaidieni hili

alichomwa moto pale kwenye bustani za reich chancellery , baadae mabaki yalienda kuzikwa, yalipozikwa yakafukuliwa tena yakachomwa moto kwa mara ya pili na mifupa ikasagwa majivu yakamwagwa mtoni

pia some accounts zinasema fuhrel alikimbia ujerumani akaenda argentina huko kwa kutumia german u boats

all in all jamaa alikuwa mtata sana, aliagiza duniani kisibaki chochote kilichokuwa chake hadi nguo zake zilichomwa moto


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hitle aliuwawa nazani na dereva wake yeye hitle mwenyewe alitoa instructions na mwili wake ukachomwa moto badae warusi walikuja kuupata wakausafirisha kwa siri mpaka kwao alikufa yeye mkewe pamoja na watoto wake

nilifuatilia stori ya ule mwili, wanasayansi walichukua skull wakapeleka maabara ikagundulika sio la hitrel kwa maana hitrel alikufa akiwa mzee lakini fuvu ni la kijana pia DNA sample haziku match na za ndugu wa hitrel


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom