"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

Mwangos aliuliwa na askar saba tena kwa bomu mchana kweupe na picha zilionyesha waliohusika lakn uchunguz ulionyesha askar hawakuhusika moja kwa moja. Je uchunguz huu polis jamii sita wenye mikanda ya polis, saa nane usiku, wala hamna picha, je uchunguz si utaonyesha polis jamii hawajahusika kabisa.
 
... walimwacha jk maana pengine naye ni p jamii! Ila ingawa kifo ni kifo wala haifurahishi; hapa pengine inafaa watu wajue kuwa, kifo cha mwangosi kimeanza kuzaa, maana auaye kwa upanga naye analiwa na upanga, walimwua mwangosi hata kutoo taarifa ilikuwa nongwa wakazidi tu kutudanganya, imekuwaje hili la mkuu wao wanakuja haraka kueleza hadhara mauwongo yao?
 
Tusipepese macho wala kuuma maneno,kamanda barlow kuna uwezekano mkubwasana kauwawa na mapolisi wenzake,kwa sababu toka amehamishiwa mwanza toka tabora amekua akifanya kazizake kwa ufanisi mkubwasana na amepunguza uhalifu na ujambazi kwa 90% ktk jiji la mwanza,sasa kuna polisi ambao wanashirikiana na majambazi ktk kufanya uhalifu,yeye kawabana hawafurukuti wameamua kummaliza,hayo yakua nakimada nikweli ila hakuuwawa kwasababu yamwanamke wamemuua kwakua anawabania ktk madiliyao,manumba safisha jeshi la polisi mwanza limeoza.
 
Fundisho kwa jeshi la polisi kufumbia macho mauaji ya raia, wamemua Mwangosi mchana kweupe kila mtu anaona, kisha wanapotosha ukweli. Sasa wapotoshe na huu pia.
 
sasa na huyo mama anapata zali la kumegwa na mkubwa the bado anaishi uswazi?
au alikuwa anafaidi kunywa bia na michemsho?
by the way so wale walomuua mwagosi ndo wamemuua bos wao au /
sielewi polisi jamii ndo wapi hao

Si huwa mnasema mafiga matatu? Huko uswazi ndio kuna figa la kwanza kama ambavyo rpc alivyo na lake
 
Time will tell!
Yatasemwa yoote
af kila mtu atachanganya na zake!!
 
Inasemekana ile system aliyoianzisha na pia alipate kuielezea last 2 days baada ya Afisa uhamiaji kunusulika kuuawa na vijana wake ndio imemtoa uhai wake.Kama nikinukuu maneno yake ya siku 2 zilizopita alisikika akisema huyu Bwana ambaye ni afisa uhamiaji aliingia kwenye mtego wa Majambazi na sie kama kawaida yetu kwa hapa Mwanza hatuchezi na majaambaazi letu ni moja ni bullet tu,na akaongeza kuwa huyu bwana anabahati sana.So inasemekana baada ya kupaki gari kwenye uchochoro ili aagane na mdada huyo kama inaavyosemekana kuwa kumbe alikuwa demu wake so viajana wake wa kazi wakaona hapa jamaa taayari kaingia kwenye anga zetu za mawindo ya maajambazi so baada ya pale kilichotokea ni kwamba vijana wale walitekeleza tu maagizo kama kawaida yao.
Na kwa bahati mbaya yule muagizaji safari hii ndio maagizo/utekelezaji umeangukia kwake.Wadau wa masuala ya kijamii wanasema hii haya yote ni Mzimu wa mwandishi wa habari aliyeuliwa na hawa hawa Police hata kama wako umbali gani lakini ndio hao hao wakutekeleza maagizo na pia waliongeza kuwa bado mengi yatatokea sana kuna Makamanda wengine kama Kamuhanda na yule wa Morogoro,Arusha wenye tabia/waliozoea kuua watu pia watakufa vifo vya ajabu vikiwemo vya kujinyonga.
Pili wakasema sasa wananchi wanasubiria kamati ingine ya Dr Imanuel Nchimbi na wakasema sasa wananchi watashuhudia Panya Na Panya wakichunguzana sasa hapo maswali ripoti itakuja vipi??????
Kwa upande wangu i dont care wauane tu pia ingekuwa safi sana kama angetangulia Kamuhanda ningefanya Party.
 
Kuna tetesi kuwa yule afisa uhamiaji ambaye ameporwa mkewe na polisi naye kapigwa nondo usiku huu na kwamba hali yake si nzuri, yuko Bugando, wana JF mlioko pale Bugando na Mwanza kwa ujumla hebu tupeni ukweli wa jambo hili.
 
Pia kuna habari za kiitelejensia nlizozipata jioni hii nikuwa kuna watu 3 muhimu wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kamanda barlow,kwa hakika kila kitu kitakua wazi nawahusika watakamatwa tu,damu ya mtu haipotei bure,labda mapolis waufiche umma kuueleza ukweli,ila mpk sasa watu 3 wako mbaroni.
 
Ifike mahara ndugu zangu pasipo kujali tofauti zetu zozote (dini, vyama nk). kufunga na kuomba kwa ajili ya viongozi wetu kwani mi naona wamekosa maadili kabisa, wezi wa mali za umma, wake za watu, waongo wao namba moja, na mungu alivyomkuu huwezi ukaficha kila ki2 siku zote

kibaya zaidi nashangaa, unakuta mtu mzima, na cheo chake anaongopa mchana kweupeeee yaan utafikiri anacheo cha kuongopa halafu wababe kweli, refer, marehemu mwenyewe juzi alipohojiwa kuhusu afisa aliyepona risasi.
 
Malipo ya kuchukua mke wa mtu hayo. Wanawake single wote hakuwaona mpaka afuate mke wa mtu?. Malipo ni hapahapa duniani.
 
Mod Tafadhali usiunganishe thread hii. Najua iko inayoripoti kifo, iko ya maswali.

Hii inahusu majibu na revelations zilizoingia kwenye dish langu.
===========

-Kamanda Barlow alikuwa na mwanamke ndani ya gari wakiwa peke yao wawili
-Mwanamke si dada yake wala ndugu yake
-Lilikuwa gari la binafsi na Kamanda aliendesha mwenyewe.
-Walitoka kwenye kikao La Kairo Hotel na siyo Florida Hotel kama IGP alivyosema katika taarifa yake
-Walipofika Kitangiri, Kamanda aliamua kumpeleka yule mama ndani kwnye uchochoro badala ya kumwacha barabarani
-Si mara ya kwanza Kamanda kumpeleka mama yule eneo lile
-Walipoingia uchochoroni, waliwakuta the so called "polisi jamii" wakiwa kwenye doria
-Kamanda alishusha kioo na kuwauliza ni kina nani, na wao walimjibu kuwa ni polisi jamii.
-Aliwahoji kwa nini wamevaa mikanda ya polisi wakati waliishazuiwa
-Ulitokea ubishi kidogo
-Kamanda akainua redio call kuwaita vijana wake waje kuwakamata
-Polisi jamii wakamdaka kumnyanganya redio call hiyo na kumpiga risasi ya shingoni
-Wakamvuta na kumlaza chini ya uvungu wa gari
-Yule mama ndiye aliyemwita mlinzi wa RPC na kumwambia aje kumchukua "mzee" maana ameuawawa
-Mama anaisaidia polisi hata sasa.

MY Take:

-Jeshi la polisi linajaribu kusafisha hali ya hewa kwa kufanya damage control
-Mme wa mama yule amekuwa akilalamika kuwa analiwa mali yake
-Kuna uwezekano, polisi jamii walijua kamanda anakuja saa ile na yule mama, na walitekeleza maagizo waliyopewa
-Kuna other underlying issues ndani ya jeshi la polisi Mwanza
-Uchunguzi hautapata ushirikiano wa kutosha kwa sababu ya chuki kubwa kati ya jamii na jeshi hilo.


wewe ni nani 1.RPC?? 2'MAMA YULE' 3. POLICE JAMII
Kama sio mmoja kati ya watajwa umejuaje yakiyojiri eneo la tukio??
 
Kuna tetesi kuwa yule afisa uhamiaji ambaye ameporwa mkewe na polisi naye kapigwa nondo usiku huu na kwamba hali yake si nzuri, yuko Bugando, wana JF mlioko pale Bugando na Mwanza kwa ujumla hebu tupeni ukweli wa jambo hili.


MAKUBWA HAYA!
Hii ndiyo staili mpya ya Kumuenzi BABA WA TAIFA!
 
Back
Top Bottom