"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

A lot of confusions on this topic. Ni aibu sana kufikia hatua hii. Wananchi wanategemea taarifa zilizo kamili na za ukweli kuhusu ni nini hakika kimetokea ili tupate funzo.

Haisaidii kutoa taarifa za uongo au zisizo kamili kama alivyosimama RC mapema na kuanza kutoa maelezo mengi unnecessary ambayo muda unavyokwenda amezua maswali mengi kuliko majibu.

Zile semina elekezi huwa hamzielewi? Katika hili mbele ya vyombo vya habari toa a brief statement ambayo haipingiki tena ukiwa na mwenye mamlaka pembeni yako nayo ni kama ifuatayo:-

"Tumestushwa kupata taarifa na imethibitika kuwa aliyekuwa RPC Afande..... amefariki dunia kutokana na kupigwa risasi (taja eneo) kama ilivyothibitishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa ambaye tunaye hapa. Vyombo vyote vya Usalama viko kazini kufanya uchunguzi wa kina kutambua sababu na mhusika/ wahusika wowote juu ya kifo hiki. Kisha tutawaeleza habari za kina wananchi na hatua zilizochukuliwa. Tunatoa pole kwa familia ya marehemu na jeshi lote la polisi. Tunawaomba muwe na subira na hakika kila kitu kitajulikana na kitawekwa wazi kwa umma wa watanzania.
 
Tetesi zinaeleza kwamba, tukio la kuuawa kwa Kamanda huyo huenda limesababishwa na uhasama na watu mbali mbali katika maeneo ya kazi alikowahi kufanyia, na kwamba hilo ni tukio linalotia shaka iwapo kama imetokea kwa bahati mbaya.

Baadhi ya watu wanalihusisha tukio hilo na mahusiano ya kimapenzi, misimamo yake mikali ya kupambana na majambazi, ambapo alikuwa akitoa onyo kwa majambazi kutoingia katika eneo lake la kazi.

Kwa upande wao, watoto wa Doroth Moses walisema kwamba siku ya tukio mama yao aliwaaga jioni kuwa anakwenda katika kikao cha harusi cha rafiki yake, na wakati anarudi nyumbani majira ya saa 4 usiku aliwapigia simu ili wamfungulie geti, na kwamba wakati mtoto mmoja Keny Rogers (17), akienda kumfungulia geti aliona kundi la watu kama watano wakiwa wamezunguka gari.

“Yule mwanaume (RPC), aliyekuwa amemleta mama (Doroth), sisi hapa hatumjui na hata hatujawai kumuoana.

Lakini mama alitupigia simu akisema tumfungulie geti..

“Wakati mimi nimeenda kufungulia geti, niliona kundi la watu watano lakini mimi hawakunioana. Wakati naendelea kuwacheki (kuwaangalia), kama nawafahamu ama lah, ghafla nikasikia mlio wa bunduki kisha wale watu wakakimbia. Nikaanza kuona damu nyingi zinamwagika chini”, alisema mtoto Keny.

Awali iliripotiwa kwamba Doroth alikua ni dada wa marehemu Barlow.

Hili ni miongoni mwa matukio makubwa ambayo yameripotiwa kutokea jijini Mwanza, ambapo hivi karibuni iliarifiwa kwamba, Ofisa mmoja wa Uhamiaji Mkoani Mwanza, Albert Buchafwe alinisurika kuuawa kwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa ni Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi cha Nyakato Mwatex (OCS), Abubakar Zebo baada ya kushukiwa kuwa ni jambazi.

Ilidaiwa kwamba, Ofisa huyo wa Uhamiaji alifyatuliwa risasi tano wakati akijaribu kukimbia, na kwamba gari lake liliumizwa vibaya na risasi zilizokuwa zikifyatuliwa na OCS Abubakar, na kwamba tukio hilo lilithibitishwa na Ofisa huyo wa Uhamiaji pamoja na marehemu RPC Barlow.

Tukio jingine lilitokea miezi michache iliyopita, ni lile la mwanasiasa maarufu jijini hapa, Seni Manumbu aliyeuawa kwa kupigwa risasi za moto na watu wasiojulikana, wakati alipokuwa akifunguliwa geti ili aingie nyumbani kwake.


Source: wavuti.com - wavuti
 
Haya sasa mi nilisema jana ,Intellejensia inabidi ichunguze vizuri jamaa asijekuwa ana kula vya watu,mambo hayo sasa nafikiri tutapata mengi zaidi,maana polisi jamii huwa hawana siraha za moto.
Mod Tafadhali usiunganishe thread hii. Najua iko inayoripoti kifo, iko ya maswali.

Hii inahusu majibu na revelations zilizoingia kwenye dish langu.
===========

-Kamanda Barlow alikuwa na mwanamke ndani ya gari wakiwa peke yao wawili
-Mwanamke si dada yake wala ndugu yake
-Lilikuwa gari la binafsi na Kamanda aliendesha mwenyewe.
-Walitoka kwenye kikao La Kairo Hotel na siyo Florida Hotel kama IGP alivyosema katika taarifa yake
-Walipofika Kitangiri, Kamanda aliamua kumpeleka yule mama ndani kwnye uchochoro badala ya kumwacha barabarani
-Si mara ya kwanza Kamanda kumpeleka mama yule eneo lile
-Walipoingia uchochoroni, waliwakuta the so called "polisi jamii" wakiwa kwenye doria
-Kamanda alishusha kioo na kuwauliza ni kina nani, na wao walimjibu kuwa ni polisi jamii.
-Aliwahoji kwa nini wamevaa mikanda ya polisi wakati waliishazuiwa
-Ulitokea ubishi kidogo
-Kamanda akainua redio call kuwaita vijana wake waje kuwakamata
-Polisi jamii wakamdaka kumnyanganya redio call hiyo na kumpiga risasi ya shingoni
-Wakamvuta na kumlaza chini ya uvungu wa gari
-Yule mama ndiye aliyemwita mlinzi wa RPC na kumwambia aje kumchukua "mzee" maana ameuawawa
-Mama anaisaidia polisi hata sasa.

MY Take:

-Jeshi la polisi linajaribu kusafisha hali ya hewa kwa kufanya damage control
-Mme wa mama yule amekuwa akilalamika kuwa analiwa mali yake
-Kuna uwezekano, polisi jamii walijua kamanda anakuja saa ile na yule mama, na walitekeleza maagizo waliyopewa
-Kuna other underlying issues ndani ya jeshi la polisi Mwanza
-Uchunguzi hautapata ushirikiano wa kutosha kwa sababu ya chuki kubwa kati ya jamii na jeshi hilo.

 
nadhani hii ni information ya uhakika... kuhusu polisi jamii wapo wengi sana mwanza..tena inaonekana vijana hao walitumia bunduki ya kamanda na kummaliza papo papo....ila ninachojiuliza kama kweli walitumwa why walimuacha huyo jike hai??

Kilio cha akina Wenje hicho... Polisi wajue kuwa hata bunduki hazina urafiki wa kudumu kwao.
 
Alikuwa hana uhusiano nzuri na JK. Tena aliwahi kuzuia mizigo ya JK
Under Riz1 control ikienda Uganda...."""""

Mtoa taarifa kasema jamaa alikuwa very strictly kwa kazi""" utiifu umemuua jamaa
!!!!!!!!
 
nadhani hii ni information ya uhakika... kuhusu polisi jamii wapo wengi sana mwanza..tena inaonekana vijana hao walitumia bunduki ya kamanda na kummaliza papo papo....ila ninachojiuliza kama kweli walitumwa why walimuacha huyo jike hai??

kwani jike alikuwa na kosa gani? afadhali wamemwacha hai akatoa taarifa, kila kitu kingekuwa gizani.
 
Risasi iliingilia juu ya bega la kushoto (upande wa abiria) na kuingia shingoni na kutokea upande wa pili. Nani aliyeifyatua? Ni abiria (Mwalimu Dorothy)? Ni 'polisi jamii' watatu waliokuwa upande huo wa gari? Maana imeripotiwa 'wavamizi' walikuwa watano; wawili walisimama upande wa dereva (Barlow) na watatu upande wa abiria (Dorothy). Mtoto aliyekuja kufungua geti kasema wale waliokuwa upande wa abiria walimpora 'mama' pochi yake, it's unlikely walipora pochi huku wanafyatua risasi. After all mgomvi wao alikuwa dereva, ndiye waliyekuwa wanazozana naye. Na pia sitarajii wafyatue risasi kuelekeza upande waliko wenzao wawili maana ingewadhuru hao wenzao. Nabaki na mwalimu Dorothy. Kuna uwezekano alifyatua yeye risasi kwa tendo la kujihami mambo yakaenda kombo. Mtu mwenye ukaribu kama huo na RPC si ajabu alishawezeshwa kumiliki bastola. Na alitumia mkono wa kulia ambao isingekuwa rahisi kwa wavamizi waliokuwa kushoto kwake kumuona ili kuepuka kunyang'anywa. Baada ya kustushwa na alichokifanya (kumuua RPC) ali-panic, na hii ikarahisisha tendo la wavamizi kumpora bastola yake na kumsachi marehemu.

Kwa kuwa hakuwepo shahidi mwingine, na ili kukwepa hatia ya 'kuua bila kukusudia', Dorothy akatunga maelezo ambayo kila anayeyasikia anashangaa.
 
Mimi nionavo hapa bila ya kutafuna maneno dada Huyu alokua nae kamanda ndio aneweza kujua mchezo wote ulivokua, je risasi alipigwa Baada ya kumuweka, au walikua wote na kabla ya kupigwa risasi kulikua na tishio lolote
 
Unasema dada yake wakati ni kimada wake? Mbona unapepesa macho?
 
WINGU ZITO:Utata wagubika kifo cha RPC Barlow, Aliye shuhudia asema kila kitu alicho kiona kabla na baada ya Kupatwa kwa mauti.


Utata umegubika mauaji ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia jana.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa Barlow, aliuawa maeneo ya Kitangiri katika barabara inayoelekea Bwiru, jirani na hoteli ya Tai Five jijini hapa. Alisema mauaji hayo yalifanyika kati ya saa 7 na saa 8 usiku, wakati Barlow akimsindikiza mwanamke aliyejulikana kama Doroth Moses. Inasemekana kuwa wote wawili, walikuwa wametoka kuhudhuria kikao cha maandalizi ya harusi ya mtoto wa dada wa Barlow, kilichofanyika hoteli ya Florida.


Hata hivyo, taarifa zisizo rasmi kutoka mitandao ya kijamii kuhusu utata wa mauaji hayo, zinaeleza kuwa Barlow na mwanamke huyo walikuwa wanatoka katika hoteli inayotajwa kwa jina la La-Kairo. Akifafanua, Ndikilo alisema Barlow alikuwa akiendesha gari yake binafsi aina ya Toyota Hilux- double cabin na kwamba alikuwa akimsindikiza mwanamke huyo kwenda nyumbani kwake.


Mwanamke huyo ambaye anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi, ni mwalimu katika Shule ya Msingi Nyamagana. Alisema wakati wakikaribia eneo la Kitangiri anakoishi mwanamke huyo, waliwaona watu wawili wakiwa wamevaa mavazi maalum (jackets) yanayovaliwa na wananchi wanaoshiriki ulinzi shirikishi unaofahamika pia kama polisi jamii. Kwa mujibu wa Ndikilo, baada ya kuwaona watu hao ambao waliwamulika kwa tochi, Doroth alimuuliza Barlow iwapo anawafahamu, naye alimjibu kuwa watakuwa ni polisi jamii.

Hata hivyo, Ndikilo alisema baada ya Barlow kusimamisha gari pembeni, mkabala na nyumba anayoishi mwanamke huyo, watu hao wawili waliwasogelea huku wakionyesha kukerwa na mwanga wa taa za gari.

Alisema watu hao walimhoji Barlow kwa nini anawamulika kwa taa za gari, lakini wakati akijaribu kutoa ufafanuzi kwamba yeye ni RPC, ghafla walitokea watu wengine wapatao watatu, walisimama kuzunguka gari la Kamanda huyo.


Baada ya kuona hali hiyo, huku akijaribu kuwauliza iwapo hawamfahamu kuwa yeye ndiye RPC na kutoa radio call (simu ya upepo) ili kufanya mawasiliano na polisi wa doria. "Ghafla mmoja wa watu hao alitoa bastola na kumfyatulia risasi ambayo iliingilia shingoni na kutokea upande wa pili wa bega," alisema Ndikilo.


Alisema baada ya tukio hilo, watu hao walichukua vitu kadhaa ikiwemo bastola, simu na radio call alivyokuwa navyo Barlow na kutoweka kusikojulikana. "Kimsingi mazingira ya mauaji yenyewe bado yana utata, lakini Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi tunafanya kazi ya kuchunguza ili kuujua ukweli,"alisema.


Kwa mujibu wa Ndikilo, baada ya kufyatuliwa risasi inaaminika Barlow alikufa papo hapo kutokana na kuvuja damu nyingi na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando ukisubiri taratibu za mazishi. Alisema kutokana na mazingira hayo ya utata ya mauaji, Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke aliyekuwa naye kwa mahoajiano zaidi. Taarifa za awali zilidai kwamba mwanamke huyo anayesadikiwa kuwa ni mjane, ni dada yake Barlow.


Lakini baadaye jana, Mkuu wa mkoa wa Mwanza alikanusha taarifa hizo na kusisitiza kuwa ni mtu ambaye alikuwa amempa lifti wakati wakitoka katika kikao cha harusi. Kufuatia mauaji hayo Ndikilo alisema kuwa Polisi Makao Makuu, limemtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba kuongeza nguvu ya uchunguzi wa tukio hilo.


Nyumbani kwa Doroth, kijana Kenrogers Edwin aliyejitambulisha kama mtoto wa kaka yake wa mwanamke huyo, alisema kabla ya tukio hilo, shangazi yake (Doroth) alipiga simu ili wamfungulie geti. Alisema kwamba wakati akifungua geti, aliona gari likiwa limeegesha huku watu wawili wakiwa upande wa abiria na wengine watatu wakiwa upande wa dereva na kisha alisikia mlio wa risasi na baadaye watu hao walitimua mbio baada ya kuona pikipiki inakuja nyuma yao.


Baadhi ya wananchi waliozungumzia mauaji hayo walielezea kushangazwa kwao na hatua ya Barlow kutembea usiku bila mlinzi wake (bodyguard) ambaye kwa kiwango kikubwa angeweza kusaidia kumuepusha na kifo.



IGP MWEMA AMTUMA DCI KWA UPEPELEZI

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Said Mwema, katika taarifa aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam, alisema ameshamtuma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Robert Manumba, mkoani humo kuimarisha ulinzi na upepelezi wa tukio hilo.

Aidha, Mwema amewaomba wananchi kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo, utakaowezesha kuwabaini wahalifu hao. Akielezea kuhusu mauaji hayo, Mwema alisema, wakati huo Barlow alikuwa akitokea kwenye kikao cha harusi ya ndugu yake eneo la Florida hoteli Mwanza mjini.

Alisema alikuwa ameongozana na ndugu yake wakitoka kwenye kikao hicho.

Alisema tukio hilo limewashtua na kuwahuzunisha na kwamba wakati uchunguzi ukiendelea, wataendelea kutoa taarifa kadri wanakavyozipata. ….


MAKAMANDA WA MIKOA WATOA KILIO

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa mbalimbali nchini, wamesema kuwa wamempoteza kiongozi mwenye uzoefu wa muda mrefu kazini na aliyekuwa mchapakazi katika jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema ukomavu wa kazi ndio uliosababisha kamanda huyo kupelekwa katika mkoa ambao ni miongoni mwa mikoa migumu nchini.


Alisema enzi za uhai wake, alikuwa akiwaelimisha wenzake ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kwamba alikuwa mwepesi kuwarekebisha wale wanaoenda kinyume na kazi. Kenyela alisema kwa upande wake atamkumbuka kwa sababu ndiye aliyempokea wakati akianza kazi hiyo na alikuwa akiishi naye kwenye kambi za maofisa huko Tabata.


"Wito wangu kwa wananchi walaani vitendo vya mauaji ya viongozi kwa sababu kumpoteza kiongozi ni gharama kubwa katika nchi hasa ukiangalia muda uliotumika kumuandaa hadi amefikia hatua hii," alisema. MOROGORO Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema kuwa, ameguswa na msiba huo wa ghafla na kueleza kuwa, atamkumbuka daima kwa kuwa alikuwa akifanya kazi yake kwa kujiamini.


"Tumempoteza jembe kwa sababu alikuwa mzoefu kwenye kazi na asiye mchoyo pindi umwombapo ushauri, kwa wale wachanga kwenye kazi walikuwa wakimtumia sana ili waweze kuifanya kazi yao kwa ufanisi," alisema.

MTWARA Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki amewataka wenzake, kuyaenzi na kuyaendeleza yale mazuri aliyokuwa akiyafanya Barlow enzi za uhai wake.



TANGA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, ameeleza kusitikitishwa na mauaji ya Barlow na kuwataka watumishi wa jeshi hilo kuwa wavumilivu wakati wakisubiri uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea ili hatua madhubuti ziweze kuchukuliwa.

"Kwa sababu kuna kikosi maalum ambacho kimeenda kufanya uchunguzi wa mauaji hayo basi nawasihi wenzangu tuendelee kuwa wavumilivu mpaka hapo upelelezi utakapokamilika na kujua hatma yake au hatua gani za kuchukua, "alisema. Alimwelezea marehemu alikuwa mtu mchapa kazi, mvumilivu na aliyeipenda kazi yake na kwamba ameacha pengo kubwa katika nafasi hiyo.



KILIMANJARO
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, amesema kifo cha Barlow ni cha kawaida ambacho kinaweza kumkuta mtu yeyote na haipaswi kujiuliza maswali mengi. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Boaz alisema kifo hicho kinaweza kikamkuta hata rais wa nchi yoyote ambaye analindwa na walinzi chungu nzima.


"Kifo chake kinatupa majonzi sisi makamanda wenzake,lakini kikubwa kilichobaki ni kumuombea kwa Mungu na kuacha uchunguzi kufanyika," alisema. Aliongeza, "kwa sasa ni mapema mno kuzungumza chochote,lakini ninachoweza kusema ni kuwa kifo chake kimenistua na ni kifo ambacho kinaweza kikamtokea mtu yeyote."


Aidha kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani Kilimanjaro wameeleza kushangazwa na kiongozi mkubwa wa Polisi kuuawa na majambazi. Bariki Sanga mkazi wa Kilimanjaro aliliambia NIPASHE Jumapili kuwa,ni jambo la kujifunza kwa kila kiongozi na kila raia kuwa mlinzi wa mali zake mwenyewe.



MBEYA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko kifo hicho. Alisema ingawa hapaswi kulitolea tamko kwa kuwa linashugulikiwa na Polisi Makao Makuu, kifo hicho ni changamoto kubwa kwa jeshi hilo ambalo sasa linatakiwa kujipanga na kufanya kazi kwa bidii. Alisema kuwa yeye binafsi anamfahamu vizuri Barlow kwa kuwa alimpokea vizuri wakati yeye (Diwani) alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoani Shinyanga.

Alisema Barlow pia alikuwa ni mwenyekiti wa Makamanda wa Polisi wa Kanda ya Ziwa ambaye alikuwa akiwaunganisha vizuri na kupunguza kabisa matukio ya uhalifu kwenye kanda hiyo. Aliongeza kuwa kwa vyovyote ambavyo uchunguzi utakavyobaini, kifo cha Barlow ni pigo kwa Polisi, kwa kuwa mchano wake ulikuwa bado unahitajika sana ndani ya jeshi hilo.



DODOMA

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma, Stephen Zelothe, ambaye Barlow alikuwa mwanafunzi wake kikazi, alisema ni masikitiko makubwa kutokea kwa tukio hilo. "Ni masikitiko makubwa kutokea kwa jambo hili…siwezi kusema lolote tuache kwanza mambo ya kidunia (mazishi) yapite,"alisema Zelothe kwa masikitiko makubwa alipoulizwa nini kifanyike

*Taarifa hii imeandaliwa na George Ramadhani, Mwanza, Romana Mallya, Dar es Salaam, Sharon Sauwa, Dodoma, Lulu George, Tanga, Charles Lyimo, Moshi na Emmanuel Lengwa,


CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


 
Kuna habari zaidi ya tatu kuhusiana na kifo cha huyo RPC; Ni Aibu MAMBO ya kipolisi kuchukuliwa kama ni SIASA. Kwa kweli SIASA za Nchi lazima zitengane na POLISI na kuiacha POLISI iwe huru; Watu wa Mwanza wengi wao hawalipendi JESHI HILO la POLISI.

KATIBA - TENGANISHA JESHI la POLISI; MAHAKAMA toka kwa Makucha ya RAIS wa CHAMA TAWALA
 
Hiyo ndio tz,kisima cha amani!Kamanda wa police wa mkoa mkubwa km mwanza anapgwa risas saa7uck,et alikua anatoka kweny kikao cha harus!Kikao mpaka muda huo!?
 
Acha uzushi mkuu,
We unaona kuna mazingira ya udada pale??

Mtoto wa yule mama (Mwl. Dorothy) anasema alimuona mama yake akija na mgeni, kama ni dada yake ina maana mtoto hamjui mjomba wake??
 
Mshahara wa dhambi ni mauti. Ndugu walimwengu naomba tujifunze kwamba Mungu hapendezwi na dhambi zetu. Ni hekima kuacha dhambi na kujitahidi kusihi kwa kufuata amri kumi za Mungu. Our duty is to obey GOD Commands,and His duty is to keep promises.
 
Duh! Wakuu! Kwa sura hii ya dada wa RPC (late), lazima mwanamume uwe kama Samson na Delila.
 
Back
Top Bottom