"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

Jamani hiyo picha siyo ya Mwl Dorothy na wala aliyoko kwenye picha siyo Mtanzania. Ni ya mwanamama wa wamerakani na ilitumika kwenye article inayohusu obesity na domestic abuse huko Marekani. Tangu jana watu wanasema hiyo picha siyo lakini bado inatumika! Mods!
 
Hiyo picha sio ya huyo mama aliekuwepo na Kamanda Barlow,someni hii link:U!Study: Obesity in black women linked to childhood abuse | theGrio
 
Ni mpenziwake na si dadayake,na huyo mama aliposhuka tu ktk gari ya kamanda, anaenda ndani ya nyumba yake akaskia majibizano ya maneno na mlio wa risasi iliyompata shingoni rpc akafa hapohapo.
 
Tetesi zinaeleza kwamba, tukio la kuuawa kwa Kamanda huyo huenda limesababishwa na uhasama na watu mbali mbali katika maeneo ya kazi alikowahi kufanyia, na kwamba hilo ni tukio linalotia shaka iwapo kama imetokea kwa bahati mbaya.

Baadhi ya watu wanalihusisha tukio hilo na mahusiano ya kimapenzi, misimamo yake mikali ya kupambana na majambazi, ambapo alikuwa akitoa onyo kwa majambazi kutoingia katika eneo lake la kazi.

Kwa upande wao, watoto wa Doroth Moses walisema kwamba siku ya tukio mama yao aliwaaga jioni kuwa anakwenda katika kikao cha harusi cha rafiki yake, na wakati anarudi nyumbani majira ya saa 4 usiku aliwapigia simu ili wamfungulie geti, na kwamba wakati mtoto mmoja Keny Rogers (17), akienda kumfungulia geti aliona kundi la watu kama watano wakiwa wamezunguka gari.

"Yule mwanaume (RPC), aliyekuwa amemleta mama (Doroth), sisi hapa hatumjui na hata hatujawai kumuoana.

Lakini mama alitupigia simu akisema tumfungulie geti..

"Wakati mimi nimeenda kufungulia geti, niliona kundi la watu watano lakini mimi hawakunioana. Wakati naendelea kuwacheki (kuwaangalia), kama nawafahamu ama lah, ghafla nikasikia mlio wa bunduki kisha wale watu wakakimbia. Nikaanza kuona damu nyingi zinamwagika chini", alisema mtoto Keny.

Awali iliripotiwa kwamba Doroth alikua ni dada wa marehemu Barlow.

Hili ni miongoni mwa matukio makubwa ambayo yameripotiwa kutokea jijini Mwanza, ambapo hivi karibuni iliarifiwa kwamba, Ofisa mmoja wa Uhamiaji Mkoani Mwanza, Albert Buchafwe alinisurika kuuawa kwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa ni Mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi cha Nyakato Mwatex (OCS), Abubakar Zebo baada ya kushukiwa kuwa ni jambazi.

Ilidaiwa kwamba, Ofisa huyo wa Uhamiaji alifyatuliwa risasi tano wakati akijaribu kukimbia, na kwamba gari lake liliumizwa vibaya na risasi zilizokuwa zikifyatuliwa na OCS Abubakar, na kwamba tukio hilo lilithibitishwa na Ofisa huyo wa Uhamiaji pamoja na marehemu RPC Barlow.

Tukio jingine lilitokea miezi michache iliyopita, ni lile la mwanasiasa maarufu jijini hapa, Seni Manumbu aliyeuawa kwa kupigwa risasi za moto na watu wasiojulikana, wakati alipokuwa akifunguliwa geti ili aingie nyumbani kwake.


Source: wavuti.com - wavuti
 

umenishawishi kuliko yeyote yule toka tukio hili litokee! Maelezo yako yana mashiko,sehemu nzuri ya kuanzia kwa watakaopeleleza mauaji haya
 
Reactions: awp

Ninashawishika sana kuamini taalifa hii sitaki hata kujua souce yake ni wapi ila ukweli umo ndani yake. Safi sana endelea kutuhabarisha.
 

kaka hebu tupe ushahidi nasi turidhike kwenye hizo red na pili polisi jamii kwa tafsiri ipi maana nijuavyo mimi polisi jamii ni sungusungu na huwa silaha yao ni marungu na mapanga, na kwanini wampige risasi

Hapo na mimi pamenishangaza sana,sungu sungu tangu lini wakatembea na bastola?
 
inasikitisha sana, amelichafua jeshi la polisi, lakini iwe fundishe kwa wengine wenye tabii hii, majina yenu tunayajua na arobaini zenu zinakaribia.
 
Waandishi wetu wa habari nao wamezidi uchakachuaji! Sijui hata kama hawa NIPASHE wataomba radhi!

ilipozama ile meli kule zenji (nungwi) mara ya kwanza achana na skagit unaikumbuka ile picha iliyokuwa inaonyeshwa ??!! tulikuwa tunaonyeshwa meli iliyozama huko brazil...ni tatizo la nchi.....
 
Du picha hata km sio ya Mwl Doroth Moses (Lyimo) lkn ujumbe umefika dude km hilo ni halali kwa RPC kumwaga zaidi ya 75,000/ za vinywaji tu bado nyama choma na room
Mkwala mwingine ule wa kuchomoa rediocall badala ya bastola wakati unajua maadui nu wengi wakiwepo waliozaanaye hata jamaa wa uhamiaji
Mwisho mwenye Bar mwanamke km naye Mchagga. Tume ya Nchimbi isiundwe kwani RPC hakuwa kazini na kumpigia mizinga /risasi wakati wa mazishi juu yenu sisi tumeshajua kisa
 
Du afadhali wanaochukua wake za watu na kukimbilia makanisani kutaka wafungishwe nao ndoa. Lakini hatuna uhakika na haya mambo ya kuletewa juu kwa juu tusubiri taarifa rasmi.
 
Japo kifo sio kizuri kwa mtu yeyote, swali ni kwamba kwanini hao makamanda wa polisi hawakutoa masikitiko yao kwa kifo cha Daud Mwangosi??? Kumbe nao yakiwafika wanajua kufa ni kubaya, sasa mbona risasi za moto nje nje kwa raia???

Tujifunze kwa matukio haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…