Kuna aina nyingi za michungwa ila hapa kwetu tuna aina zifuatatazo.
1/Early and late valensia sifa kuu ni kuwahi au kuchelewa kukomaza matunda nyakati za msimu. Kuweni makini mkiwa mnanunua miche. Uzuri valensia Ganda ni pana hivyo husafirishika kwa urahisi salama salmini na linapendwa sokoni kwa eneo kubwa.
2/ Msasa hapa limetawala mkoa wa Tanga hasa wilaya ya handeni sifa yake ni ganda laini hivyo kusafirisha Mara nyingi ni ishu.
3/ Matombo sweet ni kizazi kinachokuja kutawala sio muda mrefu ila kwa Sasa sio maarufu na halina ushabiki sana maana lina sifa ya katikati tu.
4/ George Washington ni maarufu kama Valensia kwa kuwa ni Exotic au kimataifa ila halina wapenzi wengi hasa watu wa ndani yaani wenyeji wa ndani,ganda kubwa maji kidogo.
5/ Sour Oranges ni aina ya mwisho au machungwa machachu haya sio maarufu sana ila unaweza yaona hapa Tanzania kule malamba mkoani Tanga. Yana sifa ya uchachu na yanapendwa na wahindi sana.
Mlimao ndio chanzo mama cha mimea jamii ya limao yote kwa kutoa miche ya kubebeshea (Rootstock) ikiwa na uwezo wa kukinzana na wadudu na mabadikiko ya hali ya hewa.
Baada ya walau 20-25cm unaweza kuunga au kubud (Bud ni kijicho from the point of English words not horticultural or Botanical). Mlimao unaweza kubebeshwa na mlimao kupata zisizo na mbegu (Lisbon) au zenye mbegu (Rough lemon),ndimu zenye mbegu na zisizo (Tahiti and seeded), Chungwa aina zote_dalansi,pomelo na kumquat.
Miche ya kisasa ipo na ushauri wa kilimo cha mbogamboga na matunda unatolea na huduma za kutembelea/kusimamia mashamba.
Tuma sms whatsup 0714600575.
Au sms ya kawaida 0620598113.
View attachment 1642786View attachment 1642788View attachment 1642789