Wanawake wengi ndio wanamiandiko midogo,
Miandiko Kwa sehemu kubwa inachangiwa na mambo Yafuatayo;
1. Ushikaji wa Kalamu,
2. Size ya kiganja na vidole.
3. Kalamu
4. Umri uliojifunzia kuandika.
5. Akili
6. Msawazo wa macho.
Msawazo wa macho ni vile macho yaonavyo karatasi na muandiko wakati mtu anaandika.
Ndio maana kuna ambao hawezi kuandika wakati karatasi imenyooka, wanaipindisha karatasi upande au shingo zao.
Muandiko unaosomeka unaashiria akili iliyotulia ingawaje haimaanishi kiwango cha akili.
Muandiko mcharazo unaashiria akili ambayo haijatulia, yaani inayoenda Kasi na kufikiria Kwa upesi, Sana.
Muandiko unamahusiani na tabia,
Wenye muandiko midogo kitabia huwa Wabinafsi na endapo ubinafsi ukizidi hugeuka wachoyo.
Wanawake wengi huandika miandiko midogo na hii huelezea tabia zao za ubinafsi.
Hata wanaume wenye miandiko midogo huwa Wabinafsi.
Tofauti na watu wenye miandiko mikubwa ambao hawabanii mistari kwenye karatasi.
Niishie hapa.
Taikon wa Fasihi