Heshima kwenu wakuu!
Kwanza niseme kuwa sio mtaalamu katika mambo ya magari.
Naomba kujua ukweli kuhusu ubora wa gari unavopungua kadri gari inavozidi kutembea. Ni kilometa ngapi ambazo gari ikishafika hiyo gari inakuwa imepoteza ubora wake?
Naomba ushauri hasa kwa gari aina ya Noah.
Natanguliza shukurani! [emoji122]
Umbali gari liliotembea sio issue, unavonunua gari kwa Mtanzania angalia/zingatia vitu hivi:
1. Service history. Na wengi hatunaga logbook ya service kabisa. Inabidi uwe na kitabu una record kila kitu ulichofanya/badirisha kwenye gari, tarehe na gharama yake.
2. Wamiliki waliopita. Gari kama imeshapita kwenye mikono zaidi ya 4 hatari sana. Pia ata umri status na jinsia. Magari yaliomilikiwa na vijana mengi sio well maintained na serviced. Wazee wa cheap, gereji za vichochoroni. Ndio maana madalali wetu utasikia gari alikua anatumia mwanamke au muhindi.
3. Angalia accident records. Angalia kama airbags zimewahi kulipuka au mbele chasis kama imenyooshwa. Viajali vingine vya kukwanguana na bodaboda vinavumilika. Ata rangi kama imerudiwa sio mbaya as long iko poa. Dar kurudia rangi kawaida.
4. Wewe angalia exterior na interior ya gari. Icho ndio cha kwanza. Ukiipenda test drive. Ukiridhika na uendeshaji wake, muite fundi makenika acheki sasa technical issues. Hapo jitahidi fundi asije kununuliwa na muuzaji. Wanaishara zao.
5. Gari modifications zikiwa nyingi jiulize mara mbili. Muffler, spoilers, tuned engine etc unless uwe fan au ndio vitu unavovitaka.
Hayo ni baadhi ambayo uwa tunayasahau kuyatilia maanani wakati wa kununua gari. Mengine yashasemwa sana humu.