mjasiriamali mdogo
JF-Expert Member
- Mar 15, 2013
- 258
- 110
Habari waungwana. Leo ngoja nieleze mchakato wangu wa kitambulisho changu cha taifa mpaka kupata namba na niliyoyashuhudia ofisi za NIDA.
1. Kabla sijaanza kufatilia kitambulisho cha taifa, nilianza kuuluzia nyaraka zipi zinahitajika kaambatanishwa.
Nikaambiwa cheti cha kuzaliwa,(kadi ya mpiga kura, leseni ya udereva, O au A level living certificate) n.k barua ya mtendaji. Nakala ya utambulisho wowote wa wazazi (mmoja au wote)
2. Baada ya kugundua viambatanisho vinavyohitajika na kuambiwa kuwa cheti cha kuzaliwa ni cha lazima kuliko vitu vyote hapo juu. Nakaenda RITA makao makuu posta kujiandikisha kupata cheti cha kuzaliwa, nikalipa 20000 nakaambiwa baada ya siku 14 kitakuwa tayari.
3. Baada ya siku 14 (10.9.2019) mapema sana nikaenda RITA nikiwa na fomu ya NIDA imejazwa na kupigwa mhuri wa mtendaji, barua ya mtendaji, kopi ya mpiga kura, viambatanisho vya wazazi wangu wote 2 nikakuta cheti kipo tayari, nikachukua nikaenda moja kwa moja ofisi za NIDA wilaya ya Temeke.
4. Nilikuta watu wengi sana pale ilikuwa mida ya saa 6 mchana, nikauliza taratibu zipoje hapa, wakanijibu tulia tu atakuja hapa nje na kukusanya fomu, halafu mmoja mmoja atakuwa anaitwa ndani, kweli fomu zikachukulia na baada ya muda mmojammoja anaitwa na kuulizwa madogo madogo, hususani kama fomu na nyaraka zako zina kasoro, mimi niulizwa umezaliwa wapi na lini kiuzushi tu.
Saa 10 jioni nikafanikiwa kupiga picha nakuondoka. Kabla sijaondoka nikauliza lini kitakuwa tayari, nikiambiwa baada ya miezi 2 namba itakuwa tayari sio kadi.
4. Baada ya mwezi mmoja na nusu hivi nikjaribu kwa njia ya mtandao nikapata namba. Nikawapigia simu NIDA waniambie lini kitambulisho kitakuwa tayari niende kuchukua, wakaniambia kuanzia mwezi wa 2 au 3 mwaka huu.
WENGI WANAOLALAMIKA KUHUSU NIDA WANAKUWA WANA MAPUNGUFU KWENYE NYARAKA ZAO HASA VIAMBATANISHO CHETI CHA KUZALIWA NA UTAMBULISHO WA WAZAZI. SIKU MOJA TU NILIMALIZA MCHAKATO MZIMA.