Ukweli kuhusu nyaraka kwenye kesi ya Lissu kujulikana leo

Ukweli kuhusu nyaraka kwenye kesi ya Lissu kujulikana leo

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amerudishwa tena katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Dar es salaam kwa ajili ya muendelezo wa kesi yake ya uhaini.

Kurudi kwa Lissu leo Septemba 9, kunatokana na mapingamizi aliyoyaibua jana Septemba 8, mbele ya Jopo la Majaji watatu Jaji Dunstan Ndunguru, Jaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde ambao wanasikiliza shauri hilo.

Miongoni mwa hoja za Lissu ambazo anatarajiwa kuzijengea msingi wa mapingamizi yake hii leo ni kwamba alipewa nyaraka tofauti ya mwenendo wa kesi yake kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, huku akipinga taarifa za mchakato wa ukamatwaji wake.

Katika kesi hiyo Lissu anadaiwa Aprili 3, 2025 ndani ya Jiji la Dar es salaam, anadaiwa kutoa maneno yenye nia ya kushawishi ama kuchochea umma kuzuia kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025.
1757399559247.png


 
Back
Top Bottom