UKWELI KUHUSU NYOKA MWENYE VICHWA VIWILI Je, Nyoka hawa wapo au ni hadithi tu?

UKWELI KUHUSU NYOKA MWENYE VICHWA VIWILI Je, Nyoka hawa wapo au ni hadithi tu?

badshah

Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
51
Reaction score
32
Ukweli ni kwamba nyoka mwenye vichwa viwili yupo, lakini ni wachache sana. Hawa nyoka ni kama mapacha walioungana au unaweza kusema kuwa ni nyoka mmoja mzima lakini ana vichwa viwili vilivyokaa mbadala yaani nyuma na mbele. Nyoka hawa sana sana unaweza kuwaona katika mbuga za wanyama au sehemu za kutembelea kiutalii zenye maonyesho ya wanyama wa aina mbalimbali. Baadhi ya sehemu za makumbusho wamehifadhi masalia au sampuli ya nyoka hawa wenye vichwa viwili.
 
Hadithi hizo,kwa hiyo anakula kwa kutumia pande zote?

two-headed-snake-05.jpg


snake.jpg


images
 
Mwenyewe kwa macho yangu nilimwona nyoka wa namna hii katika zoo. Hata hivyo hakuna la ajabu. Mmoja ameshaelezea hapo juu kwamba ni mapacha. Tunayaona mambo haya hata kwa binadamu. Wengine huzaliwa wawili wakichangia sehemu za viungo.
Si hadithi tupu. Na hadithi nyingi hata ngano hutokana na ukweli fulani.
 
Hizi zipo kama vile binadam anavyoweza kuzaliwa akiwa na vichwa viwili au na sehemu nyingine za mwili. Hawa naitwa conjoined twins kwa binadam sasa sijui jina halisi la hawa snake na wanyama wengine. Possible waje watu verternally medicine watueleze haya naamini wanajua zaidi kuliko mimi
 
Nenda Gangalyandefu au Lihogosa Njombe waulize wenyeji wapi anaonekana nyoka wa aina hiyo watakupeleka ukamwone :redfaces:
 
Kuna nyoka weusi wafupi maarufu kama ndumilakuwili (jina la katuni maarufu ktk gazeti la sani) hawa wapo haswa maeneo ya pwani na wana sifa y kutumia pande zote mbili kutembelea lkn si vichwa viwili upande mmoja kama picha hizo hapo juu.
 
Back
Top Bottom