Ukweli kuhusu nyota

Ukweli kuhusu nyota


NYOTA YA MASHUKE (VIRGO)

  • Hii ni nyota ya sita kwenye mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale wote ambao wamezaliwa kati ya tarehe 23 Agosti na 22 Septemba ya mwaka wowote.
  • Siku yao ya bahati ni Jumatano.
  • Namba yao ya bahati ni 5.
  • Rangi zao ya bahati ni Njano na Bluu isiyoiva.
  • Asili yao ni Udongo.
UHUSIANO WA KIMAPENZI
(MASHUKE NA SAMAKI):

Tabia ya Samaki ya fikra na ndoto za mambo ya baadae inapata faraja kubwa kwa Mashuke ambao ni wenye busara na wanaopenda kutumika na kutekeleza yale wanayotakiwa kufanya wakati wowote.
Mkuu nami naomba maelekezo ya nyota yangu.
Nimezaliwa June 9
 
Kazi kwako kuamini au kuto amini mimi hiyo sio kazi yangu. Mimi ninaamini kuwa nyota zinasema ukweli kwa Asilimia 1000%1000 sasa wewe ukiamini au usipo ziamini mimi hiyo sio kazi yangu.
Kuamini au kutoamini ni uamuzi wako, lakini mwishowe ukweli utabaki palepale kwamba astrology ni sawa na kuabudu shetani bila kujitambua.
 
Kwa mtu aliyezaliwa march 12 nyota yake ikoje?na akiwa kwenye mahusiano na mtu aliyezaliwa june 13 vipi kinyota wanaendana?
 
Mkuu nami naomba maelekezo ya nyota yangu.
Nimezaliwa June 9

NYOTA YA MAPACHA (GEMINI)


Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21 Mei na 20 Juni ya mwaka wowote.
Sayari yao ni Mercury (Attarid).
Siku yao ya bahati ni Jumatano.
Namba yao ya bahati ni 5.
Rangi yao ya bahati ni njano na bluu isiyoiva.
Asili ya nyota yao ni upepo.

KIPAJI CHA MAPACHA: (TELEPATHIC):

Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa cha kuwasiliana na watu ambao wako mbali kwa kutumia akili zao au hisia walizokuwa nazo.

TABIA ZA MAPACHA:


Watu wenye nyota hii ni watu wenye hisia kali sana ambao wanakasirika upesi, ni watu wasiotulia na wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kuzungumza na wanaweza sana kushawishi watu.
Ni watu ambao wanapenda sana mabadiliko na tofauti na wanapenda sana kujua mambo, wanapenda watu na wanapenda kujumuika na watu lakini wakati mwingine hawaeleweki. Wanapenda kusafiri sana.

TABIA YA MAPACHA KATIKA MAPENZI:
Watu wenye nyota ya Mapacha wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana , ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Ni watu wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.
Katika mapenzi, wao wanapenda vitu tofauti tofauti na wanahisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.
Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.
Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.

MATATIZO YA KIAFYA:
Nyota hii inatawala mabega, mikono, viganja na sehemu ya juu ya mbavu.
Tatizo la kutopumzika kwa sababu ya kutafuta mambo mapya ndio yanayosababisha maradhi kwa wenye nyota hii. Wanafikia mpaka hali ya kuisahau miili yao na mara nyingi wanapata matatizo ya neva kutokana na uchovu kwa mishughuliko mingi.
Matatizo yanayotokana na nyota hii ni mgonjwa kukosa pumzi (bronchitis), pumu (asthma), matatizo ya kifua, mafua, flu, ajali za mara kwa mara kwenye mikono na mabega.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA MAPACHA:
Kwa vile wenye nyota hii asili yao ni upepo na wao ni wenye kuzaliwa kwenye mawasiliano na uhusiano, wanapenda sana uhuru na uwazi katika kazi zao.
Wanapenda sana kazi ambazo zinawashughulisha na kufanya akili zao zisipumzike lakini siyo jambo hilo hilo kwa muda mrefu. Kuwa na mawasiliano na watu wengi kwa wakati mmoja ndio jambo linalopendwa na wenye nyota hii. Kazi zao hasa ni zile zinazohusiana na mambo ya utangazaji wa radio na televisheni.
Kazi ambazo zinahusika na mambo ya vitabu au uchapishaji vitabu. Kazi za kufundisha na kazi za ushauri nasaha.
Vilevile wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi za ukalimani au kazi za biashara lakini zinazohusiana na safari za nje.

FAMILIA ZA MAPACHA:
Watu wa nyota ya Mapacha ni waliochangamka na wenye hiari na wazazi wa Mapacha huingia katika msisimko wa watoto wao kwa raha.
Ni wazazi wenye furaha muda wote katika kutekeleza shughuli zao za nyumbani pamoja na kupenda kucheza na watoto wao na wana mipango mizuri na wanajua wapi wakiwapeleka watoto watafurahi.
wenye nyota hii wanathamini sana elimu na hawawezi kuishi bila mawasiliano na habari, hivyo huwa wanapenda kuwanunulia watoto wao vitabu vingi.
Tatizo linalotokea iwapo mtoto ataonyesha kwamba hapendi kusoma na watajaribu kila njia kumuweka katika njia wanayoitaka wao. Wakishindwa wanaacha.
Wazazi wa Mapacha hawawezi kuelezea jambo na hawana uvumilivu wa kun'gan'gania kwa mtoto asiyeelewa mambo.

MADINI YA MAPACHA:
Wenye nyota ya Mapacha wanatakiwa wavae madini ya Agata au kito chochote chenye rangi ya njano. Kito hicho inasemekana kinamuwezesha mvaaji awe na uwezo wa mawasiliano na ufahamu.

UHUSIANO WA KIMAPENZI:

(MAPACHA NA MSHALE)

Tabia ya Mapacha ya kupenda kufahamu na kuelewa mambo hutulizwa na tabia ya Mshale ambao ni wasomi na wenye kuelewa mambo mengi.

VYAKULA VYA MAPACHA:
Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndio vinavyotawaliwa na nyota yao. Vyakula vyenyewe ni kuku, rasiberi, karoti na uduvi.

NCHI ZA MAPACHA:
Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo inayotawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Ubelgiji na Wales, na baadhi ya miji ni London (Uingereza) na San Fransisco (Marekani).

RANGI ZA MAPACHA:
Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za njano au bluu isiyoiva ambayo inapendeza ikipakwa ndani ya nyumba.

Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 
Kwa mtu aliyezaliwa march 12 nyota yake ikoje?na akiwa kwenye mahusiano na mtu aliyezaliwa june 13 vipi kinyota wanaendana?


Kwa mtu aliyezaliwa march 12 nyota yake ikoje?

NYOTA YA SAMAKI (PISCES)


Hii ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 19 February na tarehe 20 Machi.
Sayari yao ni JUPITER (MUSHTARA)
Siku yao ya Bahati ni Alhamisi.
Namba yao ya Bahati ni 8.
Rangi yao ya Bahati ni Zambarau au Kahawia iliyochangamka.
Asili ya nyota yao ni Maji.

UHUSIANO WA KIMAPENZI
(SAMAKI NA MASHUKE)

Tabia ya Samaki ya kuwa na mbinu na mawazo ya mambo ya baadaye huenda sambamba na tabia ya Mashuke ya utekelezaji na kujishughulisha bila kuchoka.



Mtu aliyezaliwa june 13 vipi kinyota?

NYOTA YA MAPACHA (GEMINI)

Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21 Mei na 20 Juni ya mwaka wowote.
Sayari yao ni Mercury (Attarid).
Siku yao ya bahati ni Jumatano.
Namba yao ya bahati ni 5.
Rangi yao ya bahati ni njano na bluu isiyoiva.
Asili ya nyota yao ni upepo.

UHUSIANO WA KIMAPENZI:
(MAPACHA NA MSHALE)

Tabia ya Mapacha ya kupenda kufahamu na kuelewa mambo hutulizwa na tabia ya Mshale ambao ni wasomi na wenye kuelewa mambo mengi.
 
Hakika mzizi mkavu unazeeka vibaya, hujaelewa swali umeanza kuweka uchawi wako
 
Back
Top Bottom