Ukweli kuhusu tabia ya Uchepukaji

Ukweli kuhusu tabia ya Uchepukaji

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Habari za wakati huu wana Jamii Forums,

Kwa mtazamo wangu kuchepuka ni tabia ya mtu inayotokana na kuendekeza tamaa za mwili, ndiyo maana wanasaikolojia wamethiibitisha hilo kuwa [I]ONCE A CHEATER ALWAYS A CHEATER[/I].

Wanaume\Wanawake wengi hutoa sababu ya kuchepuka wakidai hawaridhishwi na mwenendo wa mahusiano yao au matatizo mengine.

Lakini ukweli ni kwamba mchepukaji ni mchepukaji haijalishi anaridhishwa au haridhishwi, Wapo Wanaume\Wanawake ambao wamekutana na matatizo kama hayo katika mahusiano lakini hawatatui tatizo hilo kwa kufanya udanganyifu katika mapenzi bali hutafuta njia mbadala itakayoua tatizo na siyo kuongeza tatizo.

Endapo mtu atafanya udanganyifu katika mahusiano, Mengi yanatarajiwa kutokea yakiwemo mimba zisizotarajiwa na za nje ya ndoa, magonjwa ya zinaa nk.

Wanaume\Wanawake ni wakati sasa sasa wa kupenda familia\Mahusiano kwa kuzijali na kukinzana na tamaa za mwili.

Matatizo\Changamoto katika familia au mahusiano hayazuiliki, Hivyo yatatuliwe kwa njia sahihi na si vinginevyo.

Asanteni.
 
Atakayeweza kutulia...ni heri zaidi - asiyeweza na awe makini na kila alifanyalo - atangulize furaha na mafanikio ya familia yake mbele..
Ndoa zina mambo mengi sana - no comment na hutupaswi kumnyooshea kidole yoyote - KIKUBWA NI KUWA NA KIASI katika kila kitu....
 
Ushauri mzuri
 
Back
Top Bottom