Ukweli kuhusu tanzania loans society

Msingi Hoja

Member
Joined
May 4, 2011
Posts
17
Reaction score
2
Ndugu wanajamiiforum,nimefuatilia kwa kina asasi hii inayojiita Tanzania Loans Society,yafuatayo nimeyabaini:

1. Namba ya simu iliyotolewa kwaajili ya tigopesa ni ya bwana LWEMBO FELIX. Namba hii haipatikani wala haipo kwenye system (Unobtainable)

2.Tanzani Loans Society SIO tawi zawa la Shirika kubwa nchini marekani liitwalo Advolticies Power Loans Society (APL Society) na SII kweli linaongwa na Rais Barack Obama. APL SOCIETY ni "American Protective League Society" ambayo imekuwa ikifanya kazi na secret societies nyingi marekani kwa utapeli.

3.Ukijisajili online wanakutumia code kabla ya kulipa then wanatumia code kama kukuridhisha hivi na code zao karibia zote zinaonekana hivi TANZ/fm/356t12360 baada ya hapo wanakuambia tumia hiyo namba kutuma pesa kama registration fee,ukituma tu hiyo namba niliiweka hapo juu haipatikani hadi tigo wamedai hiyo namba haipo active kwa maana haijapata mtu.

4. Asasi hii inayojiita Tanzania Loans Socity haijasajiliwa popote pale.

5. Wametaja ofisi zao zipo IFM jengo la utumishi wa umma chumba namba 388,wote huu ni uongo mtupu.

NB. JAMANI VITU VYA BURE VINAPONZA KWA WANAOTAKA MITEREMKO.
 
Tnx kwa taarifa. Wapenda miteremko kuweni makini, kuna kupoteza fedha zenu.
 

kwa kuwa asasi hii imetaja watu wenye dhamana kubwa kwenye nchi hii kama rais na waziri mkuu, na kwa kuwa JF in uwanja mpana kwa maana kwamba inamembers wa kada mbalimbali, ni vyema wakawataarifu watajwa na wakatolea maelezo jambo hili kwa kupitia vyombo vya habari ili umma uelewe kuhusu huu utapeli!
 
Msingi hoja

Kama mtu hajasajiriwa tigo pesa jina haliwezi kuonekana na ili atoe pesa anapewa code namba fulani na anayemtumia ndio huwa anakatwa. Huyu mtu jina lake linaonekana maana kuwa amesajiliwa. Sema TIGO wameona aibu wamemblock, lakini huyu ni subscriber halali wa tigo.
 
Ina maana hata salama jabir kwenye page yake alivyo sema ame hoji ridhiwani kikwete kwenye powe jam ya e.atv kuhusu hii kitu alidanganya?

Kama amedanganya basi amejishushia credibility yake kwa jamii!

Na kwa hili basi salama kamdharirisha rais na waziri mkuu pamoja na mtoto wa rais kama hii issue ni ya uongo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…