Ni muhimu waTanzania waelewe kinacho elekea kutokea katika kutafuta uongozi wa nchi hii, iwe ni kwa ridhaa yao au kwa kulazimishwa kukubali kuongozwa kwa nguvu.
Endapo kinachoitwa uchaguzi utafanyika hapo Oktoba kama ilivyo pangwa, kwenye mazingira ya sasa; ni kwamba uchaguzi huo utakuwa ni wa kulazimishwa na utakuwa siyo HURU wala wa HAKI. Mazingira yake yote yameandaliwa kuufanya usiwe uchaguzi wa viongozi walio chaguliwa na waTanzania.
Maandalizi hayo ni pamoja na kilicho fanyika katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024; ili kuwapata viongozi watakao hakikisha kura haramu kwa baadhi ya wagombea. Haya yalikuwa ni maandalizi ya kuhujumu uchaguzi mkuu wa Oktoba.
Ukweli mwingine ulio wazi ambao waTanzania wanapaswa kuufahamu, ni kujuwa wahusika muhimu katika uchaguzi huu. Wahusika wanaotafuta nafasi za kubaki madarakani, au kuingia madarakani.
Wanaotaka kubaki madarakani ndio wanao panga taratibu zote za uchaguzi, ili ziwahakikishie kuendelea kushika madaraka.
Lakini katika kundi hili pia ni vizuri kubainisha ni nani hasa mnufaika mkubwa, ambaye ndiye anayewapangia wenzake wote katika kundi hilo, na wao wanufaike.
Ndani ya CCM sasa hivi kuna makundi mawili. Kundi linaloendesha chama (watawala), na kundi kubwa la wanachama ambalo kwa sehemu kubwa, hadi hivi karibuni walikuwa hawajui kuwa chama chao kinaendeshwa na kundi maalum. Hili kundi maalum, ndilo linalofanya mipango yote ya chama, ili liendelee kujiimarisha ndani ya chama na serikalini, kwa kutumia chama cha CCM kwa manufaa ya kundi.
Hawa ndio watawala, siyo chama cha Mapinduzi.
Kundi la pili; ambalo ndilo ni la wanachama wenyewe; wao pia watanufaika kwenye uchaguzi huu feki, kwa kuwapata wabunge wengi; ambao siyo lazima kuwa watapatikana kwa haki; bali watatumia fursa ya mazingira hovyo yaliyo tengenezwa na kundi maalum, la watawala; akina Samia Suluhu Hassan; na wote wanao mzunguka anaowaamini yeye na kiongozi mwenzake ndani ya kundi hilo.
Kwa hiyo, ukweli ni huo. Kwamba, kundi la Samia linakihitaji sana chama cha Mainduzi kukitumia ili wabaki madarakani hata kama ni kwa kutumia nguvu; na hapo hapo, CCM kama chama kitanufaika kwa kutumiwa jina lake kuhujumu uchaguzi mzima na nchi kwa ujumla kwa kuwapata wabunge wengi wa "ndiyo Bi. Mkubwa" na waliotayari kulitumikia kundi la watawala kama tulivyoona katika Bunge lililopita.
Na endapo italazimu (kwa shinikizo la waTanzania) marekebisho muhimu yatafanyika kabla ya uchaguzi; hali iliyo elezwa hapo juu itakuwa ni tofauti sana na hali hii mpya.
Hili kundi la watawala watapoteza turufu yao ya kuishikilia CCM, na kuilazimisha kuwabakisha madarakani. CCM kama chama huru kitawapigania wateule wao kwenye nafasi mbalimbali za udiwani, ubunge na urais, kama chama; na wananchi watakuwa huru kuwachagua au kuwakataa.
Hili likitokea, CCM na wao watakuwa wamejinusuru toka kwenye makucha ya kundi la watawala, ambalo limeteka njia zote za kuhakikisha kuwa waTanzania wanakuwa mateka wao.
Uchaguzi ndani ya mazingira haya yatawapa waTanzania fursa ya kuwachagua viongozi wanao wataka wao; hata kutoka vyama vya upinzani.
Bunge litakalo patikana kwa njia hii litakuwa ni la wananchi kwelikweli.
Na kama CCM watakuwa bado wanayo matumaini na Samia Suluhu Hassan; akichuana na Tundu Lissu katika uwanja ulio sawa... Samia akivuka kihunzi hicho, atastahili heshima kwa kila mmoja wetu.
Waache waTanzania wawe HURU.
Mungu Ibariki Tanzania.