Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Kumekua na taarifa nyingi za watu kudukuliwa Akaunti zao za Whatsapp Toka Tanzania wengi wakilalamika mpaka kufikia hatua ya watu kuweza kuibiwa pesa zao, kuvujishiwa chati zao nk kupitia Whatsapp.
Sio Tanzania TU mpaka juzi tumeona nchi ya Iran iki tangaza kupitia kituo chao kikubwa cha runinga juu ya raia wao kuweza kufuta app ya Whatsapp kwenye simu zao japo kuwa Whatsapp wamekanusha juu ya kuvujisha taarifa.
Kiuwalisia kutumia mfumo wa end to end encryption ni kwamba mawasiliano unayoyafanya kupitia mtandao huo yatakua Siri ila Haimaanishi kwamba Akaunti yako haitaweza kudukuliwa.
Whatsapp ni kama mitandao mengine ya kijamii inaweza kuathiliwa na mashambulizi ya Udukuzi kupitia njia Mbalimbali. Mfano Tanzania mashambulizi mengi yanayofanywa kupitia Whatsapp ni ya kuwalaghai watumiaji kwa kuweza kuwaruhusu wahalifu wa mitandao kuweza kuingia kwenye Akaunti yako.
โ๏ธ Kupitia link Mbalimbali
โ๏ธ Kujisajili kwenye tovuti usizozijua za kupata pesa
โ๏ธ Kusambaza verification code kwa mtu usiyemjua
โ๏ธ Kupitia Whatsapp forward call Utapokea ujumbe kwenye email au kupigiwa ukipokea Kuna mashine ina tengeneza verification code ambazo zimetokana na Namba Yako ya simu na kudukuliwa taarifa zako.
โ๏ธ Kutumia Whatsapp web kwa ku scan Qr code hackers anachukua qr code fake anaiweka malicious ambayo uki scan unadukuliwa Akaunti yako.
โ๏ธ Kutumia app ya Whatsapp Gb, Fm Whatsapp, Aero Whatsapp nk.
Jihadhari unapotumia Whatsapp kufungua Kila link utakayotumiwa , kujiunga na video call au audio call groups au mtu unaweza kudukuliwa Akaunti yako.